enter-the-dragon-5.jpg

Novemba 27, 1940 alizaliwa mtaalamu wa sanaa za mapigo ya kung fu zenye asili ya China. Huyu sio mwingine ni Bruce Lee. Jina lake halisi ni Bruce Jan Fan Lee.

Alifariki dunia Julai 20, 1973 kutokana na kuugua ugonjwa wa uvimbe kwenye ubongo.

Bruce Lee alifariki dunia akiwa na miaka 32 Kowloon Tong, Hong Kong na alizikwa katika makaburi Lakeview, Ohio Cleveland nchini Marekani Julai 31, 1973, ambako wasanii mbalimbali walihudhuria akiwamo Taky Kimura, Steve McQueen, James Coburn, Chuck Norris, George Lazenby, Dan Inosanto, Peter Chin na kaka yake Robert.

Miongoni mwa sinema zilizompatia umaarufu mkubwa duniani ni ‘Enter the Dragon’ Bruce Lee anaelezwa kuwa 'fit' kuliko mwanaume yeyote.

Katika ardhi ya China inasadikika kulikua na siku maalumu ya kuazimisha siku yake. Kwa hiyo wakati Lee anazaliwa November 27 1940 ilikuwa ni mwaka wa kuazimisha siku ya Dragon kwa mujibu wa kalenda ya kichina.

Pamoja na kuzaliwa hosipitali ya China town jijini San Fransisco marekani baba yake Lee Hoi-Chuen alikuwa ni mchina asilia japo mama yake Grace alikuwa mchina anayeamini madhehebu ya Roman katoliki kutokana na mzazi mmoja kuwa Mjerumani.

Kurudi kwao Hong Kong kukazua utata kuhusu uraia wake halali, kwa sheria za Marekani wakati  huo kwa kuwa alizaliwa nchini humo, moja kwa moja alikuwa Mmarekani lakini pia Wachina walidai kuwa raia wao na Hong Kong pia.

Baba yake Bruce Lee alikuwa miongoni mwa watu waliofanya kazi za sanaa kama kuimba wakisafiri kati ya China na mji wa Canton uliokuwa Hong Kong na pia alikuwa  ni mcheza filamu, hivyo  ukamfanya awe akisafiri mara kwa mara.

Bruce Lee alikuwa na watoto wawili, wakiume na wa kike. Wa kiume aliitwa Brandon Lee aliyezaliwa 1965 na kufariki dunia mwaka 1993 kufuatia kupigwa risasi katika utengenezaji wa filamu yake ya mwisho.

Wa kike anaitwa Shannon Lee ambaye alizaliwa April 19,1969; ni mtaalamu wa mapigano kama baba yake na ni muigizaji. Shannon Lee alianza kuigiza mwaka 1993 na yuko hai hadi Leo.

Mei 10, 1973 Lee alizimia wakati wa kutengeneza filamu ya ‘Enter the Dragon’ akiwa na Golden Harvest mjini Hong Kong, ambako madaktari walimpeleka hospitalini na kugundua kuwa alikuwa na uvimbe katika ubongo.

Hali hiyo ilijirudia tena siku ya kufa kwake, ambako inadaiwa kuwa alizimia na hakuweza kuamka tena.

Siku ya kufa kwake, Lee alikuwa na miadi mjini Hong Kong na mwigizaji wa filamu za James Bond, George Lazenby, ili kubadilishana uzoefu na hatimaye waweze kutengeneza filamu.

Mke wa Bruce, Linda alikaririwa akisema Lee alikutana na Raymond Chow majira ya saa nane mchana nyumbani, wakijadiliana namna ya kuitengeneza filamu ya ‘Game of Death’.

Majadiliano hayo yalidumu kwa saa mbili hadi kumi jioni,  ndipo wakaenda kwa mwanadada wa Taiwan, Betty Ting Pei ambaye walisoma naye nchini Marekani kwa ajili ya kupitia ‘script’ ya filamu yenyewe, baada ya hapo wakaachana kila mmoja akaendelea na shughuli zake.

Akiwa kwa Ting, Bruce Lee alilalamika kuwa na maumivu ya kichwa, ambako mwanadada huyo alimpa dawa za kutuliza maumivu  na majira ya saa 1:30 usiku alikwenda kulala.

Chow aliporudi hakuweza kumwamsha tena Lee, kwani hata kwenye chakula cha jioni alichopanga kukutana na nyota wa James Bond hakwenda, ndio ikiwa mwisho wa habari za Bruce Lee.

Lee alifariki akiwa na miaka 32 Kowloon Tong, Hong Kong na alizikwa katika makaburi Lakeview, Ohio Cleveland nchini Marekani Julai 31, 1973, ambako wasanii mbalimbali walihudhuria akiwamo Taky Kimura, Steve McQueen, James Coburn, Chuck Norris, George Lazenby, Dan Inosanto, Peter Chin na kaka yake Robert.

Bruce Lee alitengeneza filamu tano kali, ambazo ni Lo Wei's The Big Boss (1971), Fist of Fury (1972), Golden Harvest's Way of the Dragon (1972), Warner Brothers' Enter the Dragon (1973), na The Game of Death iliyotoka baada ya kifo chake mwaka 1978.

Mnamo mwaka Mwanamuziki na Mbunge wa Mikumi Professor Jay wa Mitulinga aliwahi kutembelea na kutoa heshima zake katika kaburi la nyota huyo mahiri katika mapigo ya kung fu Bruce Lee na la mwanaye Brandon Lee.

 

0768671579

Add comment


Security code
Refresh