Screenshot_20210705-075141_Instagram.jpg

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba watawafunga bila kuwaogopa na kutwaa taji la pili miguuni mwao.

Julai 3 kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga. Ilikuwa ni zawadi ya mashabiki wa Yanga kutoka mguu wa Zawadi Mauya aliyefunga bao la mapema dk 12.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameweka wazi kwamba hawana mashaka na watani zao wa jadi wakikutana tena wanawafunga.

"Hatuna mashaka nao tukikutana nao Julai 25, tunawafunga tena, uzuri ni kwamba tuna timu imara na kila mmoja analitambua hilo.

"Mbinu za mwalimu wetu zinaonekana na kila mtu anakubali hivyo wakati ujao imani yangu ni kuona kwamba tunaongeza kasi zaidi na kuendelea kujiamini, mashabiki waendelee kutupa sapoti" amesema.

Mchezo huo ni wa fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Tayari Yanga ilitwaa taji moja mguuni mwa Simba lilikuwa ni lile la Mapinduzi ambalo lilifanyika huko Zanzibar.

 

0768671579

Add comment


Security code
Refresh