Rahem_Taifa_1.jpg

JOACHIM Low, Kocha Mkuu wa Ujerumani amesema kuwa huwa inatokea kwa wachezaji wazuri kutolewa katika hatua ya mtoano kutokana na makosa ambayo wanayafanya hivyo kwa kilichowatokea kwao hamna namna ya kuzuia.

Katika mchezo wa hatua ya 16 bora ndani ya Euro 2020, Ujerumani ilikubali kuona ubao wa Uwanja wa Wembley ukisoma England 2-0 Ujerumani.

Ni Raheem Sterling dk 75 alipachika bao la kwanza na lile la pili lilipachikwa na nahodha Harry Kane dk ya 86 na kuwaondoa wapinzani wao huku England ikitinga hatua ya robo fainali ambapo itakutana na Ukraine iliyoshinda mabao 2-1 Sweden

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate amesema kuwa wachezaji walitumia nguvu nyingi kusaka ushindi mbele ya timu imara jambo ambalo kwao liliwapa matunda.

England imeweza kushinda jumla ya mechi 14 na ililazimisha sare nne huku ikipoteza ushindi katika jumla ya mechi 15 ambazo wamekutana katika mashindano yote pamoja na mechi za kirafiki tangu Mei 10,1930.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh