ntibazonkizasaidi-191986866_385928516035930_7368437916341703832_n.jpg

NYOTA wa kikosi cha Yanga, Saido Ntibanzokiza amesema kuwa wana imani watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 28 ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Azam FC.

Raia huyo wa Burundi amesema:"Tunajua kwamba Biashara United ni timu imara na inafanya vizuri lakini hatutaweza kuwaacha waweze kushinda kirahisi kwani nasi tunahitaji ushindi.

"Kikubwa ni kuona kwamba tunaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa kupambana kwa mechi ambazo zimebaki kikubwa mashabiki watupe sapoti," amesema.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwa bao la Yacouba Songne ambaye alitumia pasi ya Saido.

 

 

 

0768671579

Add comment


Security code
Refresh