BRA.jpg

Mabingwa watetezi na wenyeji wa michuano ya Copa America timu ya taifa ya Brazil imeanza vyema kampeni ya kutetea ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Venezuela kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo.

Mabao ya Selcao yamefungwa na Marquinhos, Neymar Jr kwa mkwaju wa penati, na Gabriel Barbosa. Mchezo mwingine wa kundi hilo Colombia imeifunga Ecuador bao 1-0, Kwa matokeo hayo Brazil ndio wanaongoza kundi B wakiwa na alama 3 sawa na Colombia wanaoshika nafasi ya pili.

Mchezo unaofata Brazil itacheza dhidi ya Peru wakati Colombia wataminyana na Venezuela michezo hii itachezwa Juni 18.

Michuano hiyo itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo miwili ya kundi A, Saa 6:00 Usiku mabingwa wa kihistoria wa michuano hii timu ya taifa ya Argentina watacheza didi ya mabingwa mara mbili timu ya taifa ya Chile, wakati mabingwa wa michuano hii mwaka 1953 na 1979 Paraguay wataonyeshana umwamba na mabingwa wa mwaka 1963 timu ya taifa ya Bolvia mchezo huu utachezwa Saa 9:00 Usiku.

 

0768671579

Add comment


Security code
Refresh