mUANGOLA WA yANGA

IMEELEZWA kuwa Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo maarufu kama Carlinhos amevunja mkataba na klabu yake ya Yanga.

Sababu ya nyota huyo kuamua kuvunja mkataba wake huo ni kutokana na matizo ya kifamilia jambo ambalo limefanya aombe kusepa.

 

Pia nyota huyo alikuwa anasumbuliwa na majeraha jambo ambalo limemfanya ashindwe kuonyesha makeke yake kwenye mechi nyingi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mchezo wake wa mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Nelson Mandela wakati ubao uliposoma Tanzania Prisons 0-1 Yanga.

Alikuwa akitibu majeraha ya nyama za paja ambayo aliyapata kwenye mchezo huo na hakuweza kumaliza dakika zote 90.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh