UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchezo wao dhidi ya Simba ndani ya Ligi Kuu Bara ni wa kawaida tu kama ilivyo michezo mingine hawana hofu nao.


Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Oktoba 18 ila umepelekwa mbele  na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) kwa kile kilichoelezwa kuwa uwezekano wa kuwepo changamoto ya usafiri kwa wachezaji wa timu hizo mbili ambao wametwa Kwenye vikosi vyao vya Taifa kutokana na uwepo wa vikwazo kwa nchi nyingi kutokana na janga la Virusi vya Corona. 
Mechi hiyo imepelekwa mbele kwa taarifa iliyotolewa jana Oktoba 7 mpaka Novemba 7 mwaka huu Uwanja wa Mkapa,  majira ya saa 11:00 jioni.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema:"Mchezo wetu sisi dhidi ya Simba ni mchezo wa kawaida kama mechi nyingine ambazo huwa tunacheza hautupi presha kubwa katika hilo.
"Kinachoongezeka ni kwamba inakuwa dabi ila Kwenye upande wa dakika ni 90 na pointi tunazosaka ni tatu sawa na ukicheza na Namungo, Ihefu na timu nyingine hivyo tupo tayari kucheza nao na kupambana kupata pointi tatu hakuna kingine. "

Yanga ikiwa imecheza mechi tano ipo nafasi tatu na ina pointi 13 sawa  na Simba iliyo nafasi ya pili zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Yanga imefungwa bao moja na Simba imefungwa mawili na kwa upande wa kufunga, Simba imefunga mabao 14 na Yanga imefunga mabao saba tayari timu imeanza mazoezi kujiandaa na mechi zijazo.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh