Chirwa_na_Manula.PNG

LEO wakali wawili watakuwa uwanjani, Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba ambao wao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali wanaume 22 watapambana ndani ya uwanja kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

 


Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na hisia kubwa hasa ukizingatia kwamba tayari watani wa jadi wa Simba, Yanga wanasubiri mshindi tu wakutane naye.

Kila timu inauhitaji mkubwa leo kushidia ili kukutana na Yanga ambayo iliishinda Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa kwa kuifunga mabao 2-1.

Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba leo inahitaji kulipa kisasi cha kufungwa mechi mbili zote za Ligi Kuu Bara walipokutana na Simba huku Simba ikihitaji heshima pekee.

Kwa upande wa wakali wa kucheka na nyavu Azam FC wanaye Obrey Chirwa ambaye ni namba moja kwa utupiaji Azam FC. Ametupia mabao nane na pasi tatu kwenye ligi.

Simba wao wanaye Meddie Kagere ambaye ametupia mabao 19 na pasi tano za mabao ndani ya ligi hivyo vita ya leo ni ya kibabe kweli.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Cioaba amesema itakuwa mbaya wakifungwa tena leo.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema vijana wanahitaji ushindi.

Mchezo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku, mshindi tayari ameshajua atakutana na nani hivyo kila mmoja atapambana na mwisho dakika 90 zitaamua.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh