luludivatz 69630183 567685057104362 1445705139481588970 n

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan  ambaye ni ndugu na msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abas Lulu Diva ameibuka na kudai kuwa mahari ya mrembo huyo inaanza Tsh. 1,000 pekee.

Idris ambaye amejizolea umaarufu mkubwa mtandaoni kutokana na ucheshi wake, kupitia ukurasa wake wa Instagram amedai ametangaza hilo kwa niaba ya familia yao.

 


“Familia ya Sultan inatoa wito kwa yeyote atakayeweza kuwatua mzigo huu. Muda unakwenda na familia ipo tayari kukaa chini kufanya majadiliano. Mahari inaanzia buku. Hatupandi zaidi ya hapo,” ameandika Idris.

Hata hivyo Lulu Diva mwenyewe ameonyesha kutokubaliana na hilo, “Hivi ndio mmefikia huku, mmenieka kwenye mnada Idris Sultan ila ujue huwez kua Serious’.

Sanjali na hilo, Lulu Diva anafahamika kuwa na usiri sana kwenye mahusiano yake ingawa amekuwa akihusishwa na tetesi mbalimbali za kuwa kwenye mahusiano na wasanii wa hapa nchini ambazo yeye mwenyewe binafsi amekuwa akizitupilia mbali tetesi hizo.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh