KICHAPO alichopokea Kocha Mkuu wa Manchester City Pep Guardiola cha mabao 2-0 mbele ya Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford kumefungua njia kwa Liverpool kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa mapema kabla ligi haijakamilika.

Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp kwa sasa wamebakiza wiki moja kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa iwapo watashinda mechi zao mbili wakianza na Everton Machi 16 na wanaweza kutwaa ubingwa bila kucheza iwapo City atapigwa mechi zake mbili mbele ya Arsenal na Burnley.

 


Mabao ya Anthony Martial dk 30 na Scolt Mc Tominay dk 90+6 yaliwanyamazisha mashabiki wa City na kuifanya United kusepa na pointi tatu ikiwa nafasi ya tano na pointi 45 huku City ikiwa nafasi ya pili na pointi 57 kinara ni Liverpool mwenye pointi 82, United na Liverpool zimecheza mechi 29 isipokuwa City imecheza mechi 28.

Iwapo itashinda taji hilo Liverpool litakuwa ni taji lake la kwanza la Ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupita miaka 30.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh