Mchezaji nyota ambae ni attacking midfielder wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga SC Simon Msuva amejiunga na timu kubwa sana ya huko Ureno ya S.L. Benfica...

Msuva ametokea club ya Morocco ya Difaa El Jadida ambapo Yanga walimuuza nyota wao huko.

Yanga walivuna $80,000 kwenye dili ya kumuuza Msuva na wakati huo ilionekana ni deal kubwa sana.

Msuva aliifungia Yanga zaidi ya mabao 50 na kuwa mmoja wa wachezaji mahiri sana katika historian ya club ya Yanga. 

Kutokana na maelezo ya msimamizi wa Msuva Dr. Jonas Tibohora Msuva ataingia rasmi tarehe 15 January na atapelekwa Panathinaikos huko Ugiriki kwa mkopo kwa miezi 6.

Yanga haitopata senti hata moja kwenye dili ya Msuva.

Yanga walikosea au walisahau kuandika mkataba kuwa endapo Msuva atauzwa na El Jadida Yanga lazima ipate asilimia fulani ya mauzo ya mchezaji huyo.

Ni jambo la heri kwa nchi ya Tanzania na hata kwa wana-Yanga kuwa na mchezaji ambaye amechukuliwa na moja ya club kubwa sana duniani.

Benfica ni timu ambayo imevunja rekodi nyingi sana Ulaya na iliwahi kuwa na mchezaji bora sana duniani kwa Jina la Eusebio

0768671579

Add comment


Security code
Refresh