SPORTS & ENTERTAINMENT

 

 

Taifa Stars yapindua meza kibabe Benin

Screenshot_20211010-181317_Instagram.jpg

TIMU ya taifa ya Tanzania jana Oktoba 10 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Nahodha Mbwana Samata alishuhudia kijana wake Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema dakika ya 6 na lilidumu mpaka dakika ya 90.

Katika mchezo wa leo Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ilicheza kwa utulivu mkubwa na kusaka ushindi wa haraka kipindi cha kwanza na baada ya kupata ushindi kazi ya ulinzi na kushambulia kwa kushtukiza iliendelea.

Beki wa Stars, Kennedy Juma ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakitumia nguvu nyingi jambo lililopelekea akaonyeshwa kadi ya njano.

Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.

 

Taifa Stars kumfata Benin leo

tanfootball-244682881_420124962861620_8169784213728940573_n.jpg

LEO Oktoba 8 Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, inatarajia kuondoka leo saa 6 mchana kuelekea Benin kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia.

Jana, Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa, Taifa Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kupoteza pointi tatu muhimu.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2021 nchini Benin ikiwa ni vita ya kusaka pointi tatu muhimu.

Taifa Stars itaondoka na Ndege ya Air Tanzania leo na ina matumaini makubwa ya kuweza kupata ushindi licha ya kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kusema kwamba walipata nafasi na kushindwa kutumia ambazo walizipata.

"Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata hivyo kwa ajili ya mchezo wetu ujao tutapambana kufanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu," .

Kwenye Kundi J vinara ni Benin wakiwa na pointi 7 huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake ni nne.

PELE YUPO FITI KWA SASA

Pele_sasa.jpeg

GWIJI wa zamani wa Brazil, Edson Arantes ulimwengu unamtambua kwa jina la Pele amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake ipo poa.

Pele alikuwa hospitalini kwa siku sita baada ya kufanyiwa upasuaji hivi karibuni kutokana na matatizo ya kiafya huku kinachomsumbua kikiwa ni siri na sasa anaendelea vizuri.

Mchezaji huyo wa zamani wa Brazil mwenye miaka 80 alikuwa anatajwa kuwa na hali mbaya hivi karibuni na taarifa zilikuwa zinadai kwamba alikuwa akizimia mara kwa mara.

Nyota huyo anatajwa kuwa ni mshambuliaji mkubwa wa muda wote anakumbukwa zama za kucheza soka la ushindani kwa kuwa alicheza jumla ya mechi 557 na kutupia mabao 538 katika ngazi ya klabu na kwenye timu yake ya taifa ya Brazil ni jumla ya mechi 92 na alitupia mabao 77.

Pele amesema:"Marafiki zangu nasema asanteni sana kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkinitakia kila la heri. Namshukuru Mungu kwa kuwa ninaendelea vizuri na ninamshukuru kwa kunipa madakatri Dr.Fabio na Dr. Miguel kuangalia afya yangu," .

 

Timu ya Polisi Tanzania yaachana na wachezaji wake 13

Capture_2.PNG

Klabu ya Polisi Tanzania imeachana na wachezaji wake 13 baada ya Mikataba yao kuisha na klabu kufikia uwamuzi wa kutokuongeza mikataba ya kuendelea nao tena kwa msimu ujao. Wachezaji ambao hawataonekana kwenye msimu ujao wakikitumikia kikosi cha Polisi Tanzania kwenye michezo ya Ligi Kuu na ya Mashindano mengine ni:- 1. Marcel Kaheza 2. Joseph kimwaga 3. Mohhammed Bakari 4. George Mpole 5. Mohammed Yusuph 6. Emmanuel Manyanda 7. Mohammed Kassim 8. Erick Msagati 9. Ramadhani Kapele 10.Hassan Nassoro 11.Pato Ngonyani 12. Pius Buswita 13. Jimmy Shoji

Messi amwaga machozi akiaga Barcelona

WhatsApp-Image-2021-08-08-at-15.09.23-660x400.jpeg

Nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi hatimae leo afanya mkutano Nou Camp kwa ajili ya kuwaaga rasmi viongozi, wachezaji wenzake pamoja na mashabiki.

“Mkataba wangu haikuwa ishu sana ninachokijua ni kwamba nilifanya kilaninaloweza kufanya ili nibaki (Barcelona), club ilishasema hilo haliwezi kutokea sababu ya LaLiga”>>>> Messi

“Naweza kukuhakikishia kuwa nilifanya kila ninaloweza ili kubakia lakini haikuwezekana, kweli mwaka uliopita sikutaka kubaki (Barcelona) na nililisema hilo ila mwaka huu ilikuwa ni tofauti nilitaka kuendelea”>>> Messi

Messi (34) ameitumikia FC Barcelona karibia kipindi chote cha maisha yake, alianza kuichezea timu za vijana za Barcelona toka 2003 alipojiunga nayo akitokea Newell’s Old Boys ya kwao Argentina na 2004 ndio akaanza kucheza timu ya wakubwa ya Barcelona

 

 

Tunawafunga Simba Kigoma

Screenshot_20210705-075141_Instagram.jpg

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba watawafunga bila kuwaogopa na kutwaa taji la pili miguuni mwao.

Julai 3 kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga. Ilikuwa ni zawadi ya mashabiki wa Yanga kutoka mguu wa Zawadi Mauya aliyefunga bao la mapema dk 12.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameweka wazi kwamba hawana mashaka na watani zao wa jadi wakikutana tena wanawafunga.

"Hatuna mashaka nao tukikutana nao Julai 25, tunawafunga tena, uzuri ni kwamba tuna timu imara na kila mmoja analitambua hilo.

"Mbinu za mwalimu wetu zinaonekana na kila mtu anakubali hivyo wakati ujao imani yangu ni kuona kwamba tunaongeza kasi zaidi na kuendelea kujiamini, mashabiki waendelee kutupa sapoti" amesema.

Mchezo huo ni wa fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Tayari Yanga ilitwaa taji moja mguuni mwa Simba lilikuwa ni lile la Mapinduzi ambalo lilifanyika huko Zanzibar.

 

Page 1 of 75