images.jpg

Mamia ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia leo Jumamosi wameshiriki maandamano mjini Bangkok, baada ya waziri mkuu Prayut Chan-O-ocha kunusurika kura ya kutokuwa na imani naye. Zaidi ya waandamanaji 300 walikusanyika katika duka kubwa katikati mwa Bangkok licha ya mvua kubwa kunyesha. 

 

Kuelekea maandamano hayo polisi walitumia makontena makubwa kuzuia njia kuu za kuelekea eneo la maandamano. Kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi huku polisi wa kutuliza ghasia wakijiweka tayari kukabiliana na waandamanaji. 

 

Wiki hii wabunge wa Thailand walijadili hoja ya namna serikali ilivyoshughulikia janga la virusi vya corona. Waziri mkuu Prayuth na mawaziri wengine watano wameepuka kura ya kutokuwa na imani, ikiwa ni kura ya tatu ya kutaka kuiangusha serikali tangu uchaguzi wa mwaka 2019.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh