Bendera_Maroko___Morocco_Flag___Bendera_Kapal_Impor_Polyeste.jpg

Morocco inatarajiwa kufunga ubalozi wake nchini Algeria hii leo baada ya Algeria kuvunja uhusiano wake na taifa hilo la kifalme kuhusu kile ilichokitaja kuwa ni vitendo vya uadui.
 
 Duru rasmi nchini Morocco imeliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP, kwamba kuanzia leo Ijumaa, ubalozi huo utafungwa na balozi wake na wafanyakazi wote watarejeshwa nyumbani. 
 
Hata hivyo, duru hiyo imesema kuwa balozi ndogo za Morocco mjini Algiers, Oran na Sidi Belabbes zitabaki wazi.Nchi hizo mbili zimekuwa zikishutumiana kwa muda mrefu kwa kila upande kuunga mkono harakati za upinzani za upande mwengine.
 
Uungaji mkono wa Algeria kwa makundi yanayotaka kujitenga katika eneo linalozozaniwa la Sahara ya Magharibi hasa ndio sababu kuu ya msuguano na Morocco.Morocco imetaja kukatika kwa uhusiano huo wa kidiplomasia kuwa usiostahili na kwamba uamuzi huo ulizingatia visingizio vya uongo.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh