60b33211e4315

Wanafunzi 14 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kutoka chuo kikuu cha kibinafsi mnamo Aprili 20 katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria, wameachiliwa.

Kamishna wa Usalama wa Ndani na Mambo ya Ndani wa Jimbo la Kaduna Samuel Aruwan alitangaza kuachiliwa kwa wanafunzi 14 waliotekwa nyara kutoka Chuo Kikuu cha kibinafsi cha Green Field.

 

Aruwan ambaye hakutoa taarifa zaidi juu ya namna wanafunzi hao walivyoachiliwa, alieleza kuwa wasilishwa kwa familia zao.

Watu wenye silaha waliwateka nyara wanafunzi 19 katika shambulizi la Chuo Kikuu cha kibinafsi cha Green Field mnamo Aprili 20. Wanafunzi watano kati ya yao walipatikana wakiwa wamekufa karibu na chuo mnamo Aprili 23.

Gavana wa jimbo la Kaduna, Nasir Ahmad al-Rufai, alitangaza kwamba hatalipa fidia iliyodaiwa kwa ajili ya kuachiliwa kwa wanafunzi.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh