Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa nchi hiyo ipo tena kwenye mkondo sahihi, na akatoa mwito wa matrilioni ya dola kwa ajili ya kuwasaidia watu wa tabaka la kati kuanza upya maisha ya baada ya janga la corona. Matamshi hayo ameyatoa wakati akilihutubia Bunge la Marekani, na kuongeza kuwa fedha hizo pia zitawapa maisha mapya wafanyakazi ambao anasema walikuwa wamesahaulika. 

Huku akisifia mafanikio yaliyopatikana katika kampeni kabambe ya kutoa chanjo kwa umma dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, Biden ameliambia Bunge na taifa kupitia televisheni kuwa Marekani kila mara huwa inajikwamua yenyewe. 

Kuhusu sera za kigeni, Biden ambaye anaadhimisha siku 100 tangu aingie madarakani, amesisitiza kurejea kwa Marekani katika ushirikiano wa kimataifa uliokuwa umeharibiwa chini ya utawala wa Trump.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh