Zaidi ya watu elfu 341 wamelazimika kuhama makazi yao kwa sababu ya mafuriko yaliyotokea katika miezi 4 iliyopita nchini Somalia.

Kulingana na Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA), mafuriko hayo kutokana na mvua kubwa yamehangaisha maelfu ya watu.

Katika miezi 4 iliyopita, watu 341,884 walilazimika kuacha nyumba zao kutokana na mafuriko nchini.

Maeneo tajiri ya kilimo kwenye kingo za Mto Shabelle ndio yalioathirika zaidi na mafuriko hayo.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limebaini kuwa watu milioni 2.1 nchini wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh