Maambukizi yameongezeka kwa asilimia 25% na kufikia 7,375 kutoka 5,883 kwa mujibu wa shirika la kitaifa la utabiri na udhibiti wa matukio ya dharura.

Ongezeko la maambukizi limekuja wakati mamilioni ya watu wakichukua hatua zilizotangazwa siku ya Jumapili ili kudhibiti maambukizi.

Watu takribani milioni 26 mjini Lombardy na katika majimbo 14 chini ya sheria mpya ya karantini wanahitaji ruhusa maalum kusafiri.

Waziri Mkuu Giuseppe Conte pia ametangaza kufugwa kwa shule, maeneo ya kufanya mazoezi, makumbusho, nyumba za starehe na maeneo mengine yanayokusanya watu wengi.

Mazuio hayo yatadumu mpaka tarehe 3 mwezi Aprili.

 

Ongezeko hili linamaanisha kuwa Italia kwa sasa ina idadi kubwa iliyothibitishwa nje ya China, ambapo mlipuko ulianzia mwezi Desemba. Idadi hii imezidi Korea Kusini, ambayo ina idadi ya maambukizi 7,313.

Italia ni nchi mojawapo duniani yenye idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa. Virusi ni hatari sana hasa kwa wazee.

Miongoni mwa watu waliopata maambukizi hivi karibuni ni mkuu wa jeshi. Salvatore Farina alisema alijisikia vizuri na alijitenga mwenyewe kuepuka kuambukiza wengine.

Taratibu mpya za karantini zinaathiri robo ya raia wa Italia na katikati mwa mji tajiri ulio kaskazini mwa nchi hiyo ambao ni chachu ya uchumi wa nchi hiyo.

Mfumo wa afya ni changamoto mjini Lombardy, mji ulio kaskazini mwa nchi hiyo wenye watu milioni 10. Watu wamekuwa wakitibiwa kwenye kumbi za hospitali.

''Tunataka kuhakikisha afya njema kwa raia wetu. Tunaelewa kuwa hatua hizi zinahitaji kujitoa, wakati mwingine kidogo wakati mwingine kujitoa kwa kiasi kikubwa,'' Waziri Mkuu Conte alisema wakati akitangaza hatua hizo mpya.

Chini ya hatua mpya, watu hawapaswi kuingia au kutoka Lombardy.

Hatua hizo hizo zinachukuliwa Modena, Parma, Piacenza, Reggio Emilia, Rimini, Pesaro and Urbino, Alessandria, Asti, Novara, Verbano Cusio Ossola, Vercelli, Padua, Treviso and Venice.

Idara ya mambo ya Uingereza imeshauri kutosafiri bila sababu ya lazima kuelekea maeneo hayo.

Mkuu wa Shirika la Afya duniani, WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameisifu Italia kwa ''kujitoa kwao kwa dhati'' kwa kuweka mazuio. Mpaka siku ya Jumapili karibu watu 50,000 Kaskazini mwa Italia waliathirika na karantini.

Juma lililopita serikali ilitangaza kufungwa kwa shule zote na vyuo nchi nzima kwa siku 10.

 

0768671579

Add comment


Security code
Refresh