Utawala wa mpito wa Sudan umetangaza kumkabidhi Rais wa zamani Omar Al Bashir kwa mahakama ya uhalifu wa kimatiafa ICC, yenye makao makuu yake The Hague nchini Uholanzi.

Habari za kupelekwa The Hague zimetolewa baada ya mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba kati ya wajumbe wa serikali ya mpito ya Sudan na makundi ya waasi kutoka jimbo la Darfur.

Ahmed Tugod mwakilishi wa kundi la waasi la Vuguvugu la Haki na Usawa (JEM )amesema pande zote zimekubaliana kuwakabidhi raia wanne wa Sudan walofunguliwa mashtaka na ICC akiwemo aliyekuwa Rais wa Sudan Omar Bashir.

Tugod anasema, makubaliano ya kuwakabidhi watu hao hayatatekelezwa hadi pale makubaliano kamili ya amani yatakapofikiwa kati ya pande zote zinazo zozana huko Sudan .

Omar Al Bashir anakabiliwa na mashtaka ya mauwaji ya halaiki, uhalifu wa vita na uhalifu wa kibinadamu kutokana na vita vilivyotokea katika jimbo la Darfur mwaka 2003.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh