Bunge la Wawakilishi limepitisha azimio linalolenga kumzuia Rais Donald Trump kupigana vita na Iran kwa kupitisha azimio hilo kwa kura 224 dhidi ya 194.

Azimio hilo linalenga kuipa Kongresi nguvu ya kutoa kibali cha shambulio lolote dhidi ya Iran, pale tu patakapokuwa na shambulio la ghafla dhidi ya Marekani.

Mpaka sasa hakuna upande kati ya Iran na Marekani ambao umetamka kuwa utaendelea na mashambulizi.

Jumatano iliyopita, Iran ilishambulia kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Iraq baada ya Marekani kumuua Jenerali wa Iran, Qasem Soleimani.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh