Israel imeyashambulia maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza mapema leo baada ya jeshi kusema vilipuzi kadhaa vimelipuka katika eneo la mpakani na Gaza.

Jeshi la Israel na msemaji wa wizara ya afya ya Gaza Ashraf al-Qedra wamesema hakuna Mpalestina yeyote wala mwanajeshi wa Israel aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo. Mashambulizi ya mara kwa mara yameongezeka katika mpaka kati ya Israel na Gaza tangu rais wa Marekani Donald Trump alipoitangaza Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na hivyo kuibua ghadhabu miongoni mwa Wapalestina. Kundi la Hamas halijadai kuhusika na vilipuzi hivyo.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh