Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atakutana leo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baada ya Ufaransa kusema ni mapema mno kuamua iwapo hatua inatakiwa kuchukuliwa

kufuatia shambulizi dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike nchini Uingereza.

Msemaji wa Ufaransa amesema maamuzi yatapitishwa mara tu itakapodhirika Urusi ilihusika.

Ufaransa imesema leo inakubaliana na Uingereza kwamba Urusi ilihusika katika shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wake wa zamani huko England.

Wakati haya yakiarifiwa Urusi imesema bado iko tayari kushirikiana na Uingereza kuchunguza shambulizi hilo dhidi ya afisa wake wa zamani wa ujasusi. Uingereza imesema itawafukuza maafisa 23 wa kidiplomasia wa Urusi na kuiwekea vikwazo nchi hiyo kuiadhabu kwa kumtilia gesi ya sumu Skripal na mtoto wake wa kike, madai ambayo Urusi inayakanusha.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh