International news

Serikali ya Ugiriki kuanza kuruhusu Watalii June 15 2020

main qimg 453c26e89ce6c2202e4f8ee0b33f7e55

Wakati Tanzania imetangaza kufungua Viwanja vya Ndege na kukaribisha Watalii pia, Nchi ya Ugiriki ambayo ipo kusini Mashariki mwa Ulaya imesema kuanzia June 15 2020 itaruhusu Watalii kuingia Nchini humo.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis amesema kwa sasa Watalii wataoruhusiwa ni wale tu wanaotoka Nchi zenye maambukizi madogo ya ugonjwa wa COVID19 unaotokana na virusi vya corona.

 


Mitsotakis pia amesema Ndege nyingi zitaanza kuruhusiwa kuingia kwenye Nchi hiyo July 1 2020, ikumbukwe mpaka sasa Ugiriki ni miongoni mwa Mataifa ya Ulaya yenye idadi ndogo ya vifo vilivyotokana na corona ambapo ni vifo 170 na Wagonjwa 3000 wa corona.

“Tutashinda vita ya kiuchumi kama tulivyoshinda vita dhidi ya afya zetu, Watalii wataruhusiwa kuingia Nchini kwetu bila kupimwa corona na bila kuwekwa karantini lakini Wataalamu wa Afya watasimamia tahadhari zote na kwenye sehemu maarufu za Utalii vikosi vya Wataalamu wa Afya pia vitaongezwa.

Vifo vya corona Marekani vyazidi elfu 76

How to apply for a US Green Card 1

Hadi mapema leo hii vifo vitokanavyo na Virusi vya corona Nchini Marekani vimefikia 76,938 na visa 1,292,623 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza Duniani kwa wagonjwa na vifo.

WHO yakubali uchunguzi

sfdhfsdjhs

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limekubali kuanzisha uchunguzi kuhusu namna lilivyoushughulikia mzozo wa virusi vya corona, katika wakati ambapo China inaituhumu Washington kwa kukwepa wajibu wake.

Malkia Elizabeth kuongoza kumbukumbu za miaka 75 ya kumalizika vita vya pili vya dunia

 

Malkia Elizabeth wa II leo atatoa hotuba kwa njia ya televisheni kuadhimisha miaka 75 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia huku sherehe za mwaka huku zikiandamwa na kiwingu cha janga la virusi vya corona.

Taarifa kutoka Kenya visa vya Corona vyafikia 672, vifo 32

fgrthhhhh 626x400

Wizara ya Afya Kenya imesema licha ya maambukizi ya corona kufikia 672 nchini humo, wagonjwa wawili wa corona wote kutoka Mombasa wamefariki na kufanya idadi ya vifo vya Corona kufikia 32, wagonjwa wengine 32 wemepona na kufanya idadi ya waliopona Corona hadi sasa kufikia 239.

Mfalme Salman ataka nchi za G20 zishirikiane dhidi ya COVID-19

Mfalme Salman wa Saudi Arabia amewahimiza viongozi wa nchi zilizoendelea kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi, zinazounda kundi la G20, kuchukuwa hatua za ushirikiano na zenye tija, kutafuta majibu kwa mzozo wa kidunia unaosababishwa na mripuko wa virusi vya corona.

Aidha mfalme huyo amezitaka nchi wanachama wa G20, kuzisaidia nchi zinazoendelea. Wakati nchi tajiri kama Marekani zimetangaza mipango ya mabilioni ya dola ya kuupiga jeki uchumi, bado hakuna hatua zozote za pamoja zilizotangazwa na kundi la G20, ambazo zimekuwa zikikosolewa kwa kujivuta katika kutafuta sukuhisho.

 


Wito wa mfalme Salman umetolewa katika risala yake ya kuufungua mkutano wa kilele wa G20 ambao unafanyika kwa njia ya vidio leo Alhamis.

Amesema mzozo wa kibinadamu unaoendelea unahitaji suluhisho la kidunia, na kuongeza kuwa macho ya ulimwengu yanawatazama viongozi wa nchi wanachama wa kundi hilo.

Madagascar: Visa vya Corona vyaongezeka licha ya kuwepo kwa dawa

 111885005 afpmada 1
#HABARI: Idadi ya wagonjwa wa corona inaendelea kuongezeka Madagascar licha ya nchi hiyo kudai kuwa imepata ”dawa” ya mitishamba ya kukabiliana na kuponywa maradhi hayo.

Kufukia sasa nchi hiyo ina jumla ya watu 195 waliambukizwa virusi vya corona baada wagonjwa wengine wapya 35 kuripotiwa siku ya Alhamisi.

Uturuki yawaokoa wahamiaji 121 katika bahari ya Egean

Kikosi cha kulinda pwani cha Uturuki chawaokoa wahamiaji 121 katika bahari ya Egean.

Mzozo wa wahamiaji na wakimbizi  mpakani mwa Uturuki na Ugiriki,  kikosi cha kulinda pwani cha jeshi la Uturuki chafahamisha kuwaokoa wahamiaji na wakimbizi 121 katika bahari ya Egean.

Wahamiaji waliokwama majini  waliotoa ishara ya kuomba msaada na kikosi hicho  kutoa msaada katika bahari ya Egean walipokuwa wamekwama.

Wahamiaji hao walikwama walipokuwa katika boti katika   mbali ya mita kadhaa na ardhi ya Çeşme mkoani Izmir upande wa  Magharibi.

Mwanahabari wa shirika la Anadolu amefahamisha kwamba wakimbizi waliookolewa walikuwa wakielekea katika visiwa vya  Ugiriki vinavyopatikana katika bahari ya Egean.

Taarifa nyingine imefahamisha kuwa  maboti mengine  yaliokolewa yalikuwa na  raia wa Afghanistani 47, Syria 49 na 24 kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo mkoani Izmir.

Page 1 of 105