Wananchi wilayani Masasi wameonesha kuwa na matumaini makubwa ya kujipatia ajira kufuatia ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza chupa za maji safi na salama, kinachojengwa ambacho kimewekwa jiwe la msingi na mbio za Mwenge wa Uhuru.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wamesema kwa sasa vijana wengi wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa ajira kiasi cha kupelekea kuona maisha magumu lakini uwapo wa kiwanda hicho utawakomboa kuondokana na hali hiyo .

Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Benedict Macheso, alikiri kuwapo kwa fursa za ajira katika kiwanda hicho cha chupa ambacho ujenzi wake mpaka ulipofikia umegharimu sh. Bilioi 1.08 na kutarajiwa kumalizika katikati ya mwezi Septemba mwaka huu

Kwa upande wake, Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima, amewataka vijana watakaopata nafasi za kuajiriwa kiwandani hapo kufanya kazi kwa juhudi na kuwa waaminifu ili kampuni ipate mafanikio ambayo yatasababisha fursa ya kuongeza viwanda vingine.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh