b0c2f7fd-b93d-4937-8bde-b6a738c4aa55.jpg

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amewagiza Waganga Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanatoa taarifa za vifo vinavyotokea kwenye maeneo yao kwa lengo la kuiwezesha Kamati ya Kitaifa ya Ufuatiliaji kutathimini kama vifo hivyo vimesababishwa na uzembe wa kutowajibika ipasavyo wakati wa kutoa huduma ili waliohusika na uzembe huo wawajibishwe kwa mujibu wa sheria kupitia mabaraza ya kitaaluma.

 

Agizo hilo amelitoa Jijini Dodoma alipotembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa Sekta ya afya uliozinduliwa Julai 2021 eneo la kipaumbele cha kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambavyo vimeendelea kuwa changamoto. Dkt. Gwajima amesema tafiti zinaonyesha vifo vitokanavyo na uzazi vinazuilika na pia Serikali inafanya jitihada za kusogeza huduma kwa jamii lakini bado kasi ya kupunguza vifo hivyo hairidhishi.

 

Dkt.Gwajima amesema kuwa, ili kukabiliana na hali hiyo Wizara ya Afya kuanzia tarehe 20 Desemba 2021 itaanza kufanya vikao vya ufuatiliaji kwa njia ya mikutano kupitia mitandao kwa kuunganisha Kamati za Wizara, Mikoa na Watendaji waliopo kwenye vituo kilipotokea kifo husika ndani ya saa 24 kwa lengo la kubaini kama kifo hicho kingeweza kuzuilika ili kama kuna uzembe wa kutowajibika ipasavyo, wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria vya taaluma yao.

 

Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wafawidhi wa hospitali za mikoa hapa nchini, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest ameahidi kupitia umoja wao watahakikisha wanasimamia kikamilifu utoaji wa huduma bora ili kupunguza vifo vya uzazi visitokee ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuwahi kwenye vituo vya kutoa huduma za Afya wakati wa kujifungua huku wananchi wakipongeza serikali kwa kuboresha huduma za Afya.

v

0768671579

Add comment


Security code
Refresh