245609854 1036699790492585 8473095885413468657 n
Wakulima wa korosho kutoka wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara wamekubali kuuza korosho zao tani 3124 kwa bei ya juu ya shilingi 2401 na bei ya chini shilingi 2250 kwa kilo moja ya korosho daraja la kwanza ghafi.

Mnada huo wa pili wa mauzo ya korosho umefanyika katika MATOGORO AMCOS Tandahimba ambapo korosho zilizo uzwa ni kutoka Ghala la TANECU Tandahimba na Newala kutoka kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tanecu.

Wakulima hao wamesema Mnada umeanza kwa bei nzuri hivyo hawaoni sababu ya kuacha kuuza korosho zao.

Mnada huo umehudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala ambaye amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia ubora wa korosho zinazo letwa maghalani ili kudhibiti ubora wa Korosho.

Kanali Patrick Sawala amesititiza kuwa serikali haita mvumilia mkulima yoyote atakae changanya kurosho safi na chafu kwani kufanya hivo ni kinyume cha sheria.

Mnada wa tatu wa korosho kutoka Chama Kikuu cha Ushirika cha Tanecu unatarajia kufanyika Kitangali. Oktoba 23 mwaka huu katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh