6.jpg

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze ahakikishe mpaka kufikia Jumamosi, Oktoba 16, 2021 dawa ziwe zimepatikana katika maeneo yote nchini.

Waziri Mkuu amesema kuwa ni maelekezo ya Serikali kuwa vituo vyote vya kutolea huduma zikiwamo zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, hospitali za rufaa za mikoa lazima zipate dawa kwa kuwa zinategemea MSD

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Oktoba 10, 2021) alipokutana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze, Jijini Dodoma

 

Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa Taasisi hiyo wahakikishe wanapeleka malori 10 ya dawa katika kila kanda lengo ni kuwezesa upatikanaji wa dawa ili kurahisisha utoaji wa huduma.

 

0768671579

Add comment


Security code
Refresh