WhatsApp_Image_2021-09-08_at_15.32.45.jpeg

 Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara mikindani imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni sabini mia tano sabini na nne elfu kwa vikundi vinane vya wajasiriamali vinavyojishugulisha na biashara ndogondogo katika soko kuu la chuno mkoani Mtwara.
Akizungumza katika makabidhiano hayo mgeni rasmi kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara mh. Dunstan Kyobya amewaomba wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo kwa kuunda vikundi vyao ili waweze kupata mikopo na kuendeleza biashara zao.
Aidha Mh Kyobya ametoa wito kwa TBS na SIDO kuwatembelea wafanya biashara wa soko hilo mara kwa mara ili kutoa semina kwa wajasiriamali ili waweze kutumia mikopo yao vizuri na kuendesha biashara zao kisasa zaidi.
Juliana Manyama ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii katika halmashauri hiyo afisa maendeleo ya jamii anasema serikali wametoa elimu ya kutosha na wataendelea kufanya hivyo kwa vikundi mbalimbali ili kuweza kutambua namna ya kutumia mikopo.
Kwa upande wao wajasiria mali hao ambao ni wanufaika wa mkopo huo wanamategemeo makubwa ya kukuza biashara zao baada ya kupata mkopo huo huku wakiviomba vyombo vya habari kulitangaza soko hilo.
Vikundi saba vya akina mama na kikundi kimoja cha vijana, huku zaidi ya milioni 50 zikienda kwa wanawake.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh