Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho   amesema ujenzi wa  Meli ya Mv Mwanza Hapakazi tu ambao hadi sasa umefikia asilimia 74 utakamilika baadaye mwakani.

 
Waziri Chamuriho ameyasema hayo leo jijini Mwanza alipokuwa akikagua ujenzi wa meli hiyo ya kisasa  inayojengwa na Kampuni ya Gas Ente kutoka Korea ya kusini ikishirikiana na Kaang Nam Corperation pamoja na Suma JKT. Aidha Waziri Chamuriho amesema ujenzi wa meli hiyo ni moja  ya miradi mikubwa minne inayotekelezwa na   kampuni ya huduma za Meli  Nchini (MSCL) na kusimamiwa na  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. 
0768671579

Add comment


Security code
Refresh