Aliyekuwa Meneja wa marehemu rapa #DMX, Steve Rifkind amethibitisha kuwa zoezi la kuaga mwili wa DMX limepangwa kufanyika katika ukumbi wa Barclays Center mjini Brooklyn New York, April 24 mwaka huu.

Siku itakayofuata (April 25), familia ya #DMX na marafiki zake wa karibu watasheherekea maisha ya rapa huyo kwenye mazishi ya faragha ambayo yatafanyika Kanisani mjini New York.

#DMX alifariki dunia April 9 mwaka huu katika hospitali ya White Plains kufuatia kulazwa kwa takribani wiki moja mara baada ya kupata shambulio la moyo kwa kuzidisha dawa za kulevya akiwa nyumbani kwake.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh