Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Simon Sirro na Kamanda mkuu wa Polisi wa Jamhuri ya Msumbiji Bernardino Rafael wamekutana leo Mkoani Mtwara na kuzungumzia hali ya usalama katika eneo la mpaka baina ya nchi hizo mbili ambako kumekuwa kukitokea matukio ya uhalifu na machafuko mara kwa mara yanayodaiwa kufanywa na makundi ya kigaidi yenye itikadi za kidini.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha ndani kilichodumu kwa muda wa masaa matatu viongozi hao wamesema kuwa wamekubaliana mambo mengi ikiwa pamoja na kuendesha oparesheni za kijeshi na kubadilishana taarifa ili kuhakikisha wanawanasa wahaalifu hao.

Akianza kuongea juu ya kile walichokubaliana IGP mwenyeji Simon Sirro amesema kuwa wamejipanga vizuri na kujihimarisha ipasavyo na kuahidi kuwa haitachukuwa muda mrefu watawashughulikia, huku akiwataka wananchi waliokimbia maeneo yao katika vijijini vya mpakani kurudi na kuendelea na shughuli zao.

Kutokana na kundi kubwa la vijana wa Tanzania kudaiwa kujiunga na makundi hayo ya kigaidi yenye itikadi za kidini, Sirro amewataka wazazi kujitahidi kuwaonya watoto wao kwa kuwa hawatawaacha salama na kula nao sahani moja.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh