W
akulima wa zao la Korosho wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi, Mtwara Co-operative Union-MAMCU, wamekubali kuuza Korosho zao kwa bei ya juu ya Shilingi 2,607 na bei ya chini shilingi 2,439 kwa Korosho zilizopo katika Maghala ya Micronix, Ketikamba na Mtandi Masasi.

Kulingana na Meneja wa Mkuu wa MAMCU Ndug. Potency Rwiza amesema kuwa korosho kilo 5,526,113 Milion zimeuzwa kati ya kilo 6,975,897 Milion zilizokusanywa.

Aidha Rwiza amefafanua kuwa zaidi ya kampuni 40 zimeonesha nia ya kununua korosho ingawa ni kampuni 14 tu zilizoweka kinga ya dhamana katika msimu huu.

Akizungumza katika mnada huo Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba amesema kuwa msimu wa mwaka 2020/2021 umeweka historia katika mauzo ya korosho baada ya kutumika kwa mfumo wa aina mbili wa kawaida na wa kidigitali.

Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wakulima wanauza korosho zao zote na kupata bei nzuri sokoni ndio maana serikali ikaja na njia mbili ili nchi ambazo mipaka yake imefungwa ziweze kuagiza korosho hizo kwa njia ya mtandao.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh