Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Kimanta amewataka wanawake kushiriki katika masuala ya siasa na uongozi ili kuweza kuibadilisha jamii kwa kuwa wanawake wana uwezo mkubwa katika masuala ya uongozi kuanzia ngazi ya familia na nguzo ya mabadiliko.

Rc Kimanta ameyazungumza hayo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa mradi wa wanawake katika uongozi na ushiriki katika siasa ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania(TAMWA) na Kuwakutanisha Waandishi wa Habari 50 kutoka Mikoa 17 nchini.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwasihi Waandishi wa Habari kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya dunia katika Tasnia ya Uandishi wa Habari.
0768671579

Add comment


Security code
Refresh