Rais Magufuli leo March 13, 2020 amezindua karakana ya matengenezo ya magari na mafunzo ya ufundi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo DSM, “Karakana hii kubwa na ya kisasa imejengwa kwa ufadhili wa marafiki zetu wa Ujerumani kwa gharama ya Tsh. Bil 8.5”

“Naishukuru sana Serikali ya Ujerumani kwa kufadhili ujenzi wa karakana hii ya kisasa ya matengenezo ya magari na mafunzo ya ufundi ya JWTZ, nawashukuru pia Ujerumani kwa misaada na ushirikiano mkubwa wanaoendelea kutoa kwa Nchi yetu katika sekta mbalimbali”- JPM

“Nitoe wito kwa JWTZ kutumia vizuri karakana hii, vitunzeni vifaa ambavyo tumekabidhiwa na Serikali ya Ujerumani na ambavyo vitaendelea kuja, muhimu zaidi hakikisheni mnatumia vizuri karakana ili iwe chachu ya kuwaimarisha kiufundi na kuchochea maendeleo“-JPM

“Karakana hii itatumika kutengeneza magari yetu ya kijeshi na pia kutoa mafunzo kwa mafundi, hii itasaidia kupunguza gharama kwa jeshi letu pamoja na kuwaongezea uwezo wa kiufundi wanajeshi wetu”-JPM

0768671579

Add comment


Security code
Refresh