Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itasoma hukumu ya Viongozi wa CHADEMA Saa saba na nusu mchana leo badala ya Saa nne na nusu asubuhi.

Mahakama imefurika wafuasi wa Chadema na ulinzi umeimarishwa kwa askari kila kona kabla ya muda wa hukumu, Wafuasi hao walianza kumiminika eneo la mahakama tangu saa moja asubuhi wakisubiri hukumu ya vigogo wa Chadema akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018 na Hakimu ambaye sasa ni Jaji, Wilbard Mashauri.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh