Mkuu wa wilaya ya Newala Mh Aziza Mangosongo amewataka wazazi wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 kuwapeleka watoto wao mpema katika shule walizopangiwa.

Hayo amezungumza jana na wakazi wa kijiji cha mkunya mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea shule ya sec malegesi na shule ya sec kusini zilizopo halmashauri ya mji Newala

Aidha ameweza kutaja takwimu za shule hizo ambapo katika shule ya sec Malegesi watoto walizopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni 218 na mpaka sasa walioripoti ni wanafunzi 50 pekee, huku shule ya sec kusini wakipangiwa watoto 120 na walioripoti shuleni ni watoto 18 pekee

Mh Mangosongo ameeleza kuwepo kwa hali kama hiyo pia katika shule zingine nyingi za sec hivyo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wait shule hata wasipokuwa na sare za shule

0768671579

Add comment


Security code
Refresh