Kambi za kijeshi za Marekani zashambuliwa kwa makombora Iraq

 

Iran imefanya mashambulio ya makombora dhidi ya ngome za kijeshi za Marekani nchini Iraq kama hatua ya kilipiza kisasi mauaji ya jenerali Qasem Soleimani .

Makombora kadhaa yaliyorusha kutoka Iran yalilenga eneo la Irbil na Al Asad, magharibi mwa mji wa Baghdad.

Runinga ya kitaifa ya Iran imetangaza kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu Qasem Soleimani aliyeuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani mjini Baghdad, kufuatia agizo la rais wa Marekani Donald Trump.

Rais Trump ameandika katika Twitter yake akisema kwamba mambo ni shwari na kuongeza kuwa nchi yake kwa sasa inatathmini kiwango cha athari ya mashambulio hayo.

Kambi hizo mbili za kijeshi za nchini Iraq ambayo ni makao ya vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani zililengwa- moja ya Al Asad na nyingine mjini Irbil zilishambuliwa saa kadhaa baada ya mazishi ya Soleimani.

Kambi ya Al Asad- ambayo iko mkoa wa Anbar magahribi mwa Iraq - ilishambuliwa na makombora karibu sita.

Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei amesema shambulio hilo lilikuwa "kofi la usoni" kwa Marekani.

"Tukizungumzia makabiliano ya kijeshi shambulio hili halitoshi. Cha msingi kwa sasa ni kuhakikisha uwepo wa kifisadi wa Marekani lazima ufike mwisho," alisema.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh