Serikali imesema imefuta tozo la asilimia 15 ya bei dira kwa wakulima wa zao la korosho na badala yake tozo hiyo itakuwa inalipwa na mfuko wa WAKFU ambao unasimamia maendeleo ya zao la korosho hapa nchini.

Hayo yamesema Bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tandahimba kupitia chama cha wananchi CUF Katani Ahmadi Katani aliyetaka kujuwa serikali inamkakati gani wa kumuondolea mkulima tozo la asilimia 15 ya bei ya soko la korosho.

Akijibu swali hilo waziri mkuu amesema kuwa tayari serikali imeamua kuwaondolea tozo la asilimia 15 wakulima na kuielekeza tozo hiyo kwa Mfuko wa WAKFU kwa kuwa umekuwa ukichangiwa tozo za korosho zinazouzwa nje ya nchi kwa asilimia 65 na kwa sasa mfuko huo umekuwa na pesa ya kutosha.

Majaliwa amesema kwa kuwa mfuko wa WAKFU umeundwa na wadau wenyewe kwa ajili ya kusimamia na kuboresha uzalishaji wa zao la kororsho bado unajukumu la kuhakikisha upatikanaji wa masoko, wakulima kupata pembejeo na mbegu, kusimamia uboreshaji na kupanua mashamba ya korosho pamoja na kugharamia tafiti mbalimbali ambazo zinatakiwa kufanywa kwa ajili ya kupata ubora wa zao la korosho.

Mwezi wa April mwaka huu waziri Mkuu akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi katika Wilaya ya Ruangwa aliwaambia wananchi kuwa serikali ipo njiani kuufanyia marekebisho mfumo wa stakabadhi ghalani sambamba na kuviondoa vipengele ambavyo vilikuwa vinaonekana kuwakandamiza wakulima ambavyo ni ushuru wa asilimia moja inayokwenda kwa Afisa Ushirika wa Mkoa, Ushuru wa kusafirisha korosho kwenda Maghalani wa sh 50 kwa kg moja, makato ya sh 50 ya chama kikuu cha ushirika, riba ya Mkopo wa Benki baada ya chama kupata Mkopo na Benki Makato hayo yote yameondolewa .

Waziri Mkuu alisema kuwa hakuna haya ya kumbebesha Mkulima kulipa gharama hizo kwani kuna baadhi ya vyama vinatumia magari ya vyama kusafirishia korosho mpaka maghala makuu lakini mzigo wa kulipa gharama hizo wanabebeshwa wakulima.

Akizungumzia kuhusu riba ya Mikopo ya Benki kwa vyama vya msingi alisema sio lazima gharama hizo kufanywa na Mkulima kwani vinavyoingia Mikataba ya Mikopo hiyo ni Vyama sio wakulima hivyo vyama vinatakiwa kulipa gharama hizo.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh