Local News

Rais wa Zanzibar kupokea Airbus mbili leo

23fd6911-9575-4a56-8955-87028470c1fc.jpg

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi atapokea ndege mbili mpya aina ya Airbus zitakazowasili leo Ijumaa Oktoba 8, 2021 visiwani Zanzibar.

 

Ndege hizo mpya moja itapewa jina la Zanzibar na nyingine Tanzanite.

“Ndege hizi zina mfumo wa kisasa na zimeongezewa uzito hasa wakati wa kuruka kutoka Tani 67 hadi kufikia tani 69.9 lakini pia ina viti vya kisasa ambavyo vitawafanya abiria kustarehe zaidi” amesema Profesa Mbarawa.

Ujio wa ndege hizo utaifanya Tanzania sasa kuwa na ndege 11.

Amefafanua kuwa, pia ndege hizo zitakuwa na burudani za watoto, muziki, sinema na internet na hivyo kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwa maendeleo ya nchi

Chikota: Zilizishwi na huduma ya maji jimboni kwangu

Wakazi zaidi ya 2000 wa kijiji cha Navikole kata ya chawi halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama hali ambayo inayoinasababisha kutumia maji ya kuokoteza katika dimbwi moja linalotumiwa na vitongoji vinne.

Wamesema wamelazimika kuwekeana zamu ya uchotaji wa maji kwa siku moja kwa kila kitongoji.

Mbunge wa jimbo la Nanyamba,Mkoani Mtwara anasema bado haridhishwi na upatikanaji wa huduma ya maji hali inayomlazimu kuja na mikakati ya kuweza kulinusuru jimbo hilo ambapo anaeleza njia pekee ya kuondokana na changamoto hiyo ni kuanza kutoa maji katika mto Ruvuma

Kwa upande wake wakala wa uchimbaji wa visima na mabwawa (DDCA) Idrisa Shabani amesema wameanza kuchimba kisima katika kijiji hicho ambacho kitapunguza changamoto ya upatikanaji.

CHIKOTA APOKELEWA KWA SHANGWE JIMBONI KWAKWE

WhatsApp_Image_2021-10-06_at_17.45.36.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mkoani Mtwara Mh Abdallah Dadi Chikota akipokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi alipo fanya ziara ya kutembelea baadhi ya vijiji vilivyopo jimboni. Lengo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbali mbali zinazo wakabili wakazi wa jimboni kwakwe.

NHC kujenga majengo ya wizara ya utamaduni, sanaa na michezo

Capture.PNG

Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo imesaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Wizara hiyo kwa awamu ya pili lenye ghorofa sita na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jingo litakalojengwa eneo la Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini leo Septemba 22, 2021 jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amesema jengo hilo litakuwa na ofisi za kisasa pamoja na mahitaji yote yanayohusika katika sekta za Sanaa, Utamaduni na Michezo.

“Jengo hili litakuwa la kihistoria kwa kuwa Wizara hii haijawahi kumiliki jengo la hadhi hii, matarajio yetu jengo hili litakuwa kichocheo cha sekta hizo kutoa huduma bora na stahili kwa wadau wa sekta na wanananchi kwa ujumla” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo ambazo ni shilingi Bilioni 22.843 huku ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24.

Katibu Mkuu Dkt. Abassi amewahimiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao ni watekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo pamoja Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ni wasanifu na wabunifu wa majengo hayo wakamilisha mradi huo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa kwa kuwa wao ni mabingwa wameaminiwa kwa uzoefu wao katika masuala ya ujenzi.

 

WAFANYABIASHARA WALISUSIA SOKO LA CHUNO

WhatsApp_Image_2021-10-04_at_13.10.18.jpeg

Breaking news

Wafanyabiashara wa soko la Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani leo wameamua kuchukua uamuzi wa kuhamisha biashara zao na kurejea katika Sabasaba ambao walikuwa wakifanya mwanzo.
Wakizungumza na Safari Media wafanyabiashara hao wamedai kuwa uamuzi huo wameuchukua baada ya kukosekana kwa wateja.

Zulfa Juma na upendo Namahala wamedai kumekuwa hali mbaya ya biashara jambo linalopelekea mitaji yao kufa.

Katika hatua nyingine wanadai kutopendezwa na matamko ya viongozi wa Serikali juu ya wafanya biashara.

Safari Media ilivyomtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Kanali Emmanuel Mwaigobeko amesema hawezi kumzuwia mtu kuhama ila atalifanyia kazi.

Endelea kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii

PELE YUPO FITI KWA SASA

WhatsApp_Image_2021-09-08_at_15.32.45.jpeg

 Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara mikindani imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni sabini mia tano sabini na nne elfu kwa vikundi vinane vya wajasiriamali vinavyojishugulisha na biashara ndogondogo katika soko kuu la chuno mkoani Mtwara.
Akizungumza katika makabidhiano hayo mgeni rasmi kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara mh. Dunstan Kyobya amewaomba wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo kwa kuunda vikundi vyao ili waweze kupata mikopo na kuendeleza biashara zao.
Aidha Mh Kyobya ametoa wito kwa TBS na SIDO kuwatembelea wafanya biashara wa soko hilo mara kwa mara ili kutoa semina kwa wajasiriamali ili waweze kutumia mikopo yao vizuri na kuendesha biashara zao kisasa zaidi.
Juliana Manyama ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii katika halmashauri hiyo afisa maendeleo ya jamii anasema serikali wametoa elimu ya kutosha na wataendelea kufanya hivyo kwa vikundi mbalimbali ili kuweza kutambua namna ya kutumia mikopo.
Kwa upande wao wajasiria mali hao ambao ni wanufaika wa mkopo huo wanamategemeo makubwa ya kukuza biashara zao baada ya kupata mkopo huo huku wakiviomba vyombo vya habari kulitangaza soko hilo.
Vikundi saba vya akina mama na kikundi kimoja cha vijana, huku zaidi ya milioni 50 zikienda kwa wanawake.

HOSPITALI YA RUFAA KUANZA KUFANYA KAZI

2854269_IMG_20210722_222532_066.jpg

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini iliyopo Mitengo Mkoani Mtwara itaanza kutoa huduma Oktoba Mosi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mambo muhimu kama dawa na vifaa tiba tayari vimewasili. Watumishi 42 wa kada mbalimbali pia wamesha wasili kuanza kutoa huduma kuanzia kesho (Oktoba 1).

 

 

Page 2 of 184