Local News

MADEREVA BODABODA MTWARA KUANZISHIWA LIGI YAO

66c835f06e803896397e23232a7026e6.jpg
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara inatarajia kuanzisha mashindano ya ligi ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wa halmashauri zote za mkoa, huku lengo likiwa ni kutambua changamoto wanazokumbana nazo kwenye utendaji wa kazi zao.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ambapo amasema kuwa mashindano hayo yataanza septemba 15 na kumaliza novemba 5 mwaka huu, na yatafanyika katika Halmashauri tatu ambazo ni Mtwara, Newala na Masasi.
Byakanwa amefafanua kuwa kila halmashauri itawakilishwa na timu moja licha ya kuwa zipo zitakazowakilishwa na timu zaidi ya moja.
Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atapata zawadi ya fedha shilingi milion 2,500,000, mshindi wa pili milion 1,500,000 na mshindi wa tatu milion 1,000,000.

WAGOMBEA WENGINE 13 WASHINDA RUFAA

WhatsApp_Image_2020-09-09_at_8.33.47_PM_1.jpeg
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini imechambua rufaa zingine 34 za ubunge kati ya hizo, 13 imewarejesha kugombea ubunge, 21 imezikataa.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera imesema rufaa hizo 13 zinahusu majimbo ya Singida Magharibi, Madaba. Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene na Kigamboni.

Amesema, NEC imekataa rufaa saba za wagombea ambao hawakuteuliwa kutoka majimbo ya Singida Magharibi, Bahi, Handeni Vijijini, Madaba, Singida Mashariki, Ileje, Meatu na Bukene.

Amesema, tume hiyo baada ya uchambuzi, imekataa rufaa 14 za kupinga walioteuliwa kutoka majimbo ya Mwanga, Mafinga, Ilala, Manonga, Igunga na Kisesa

RPC Morogoro afunguka ajali ya Kontena kukandamiza Costa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa jumla ya watu 10 wamejeruhiwa huku 4 kati yao wakijeruhiwa vibaya, baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kukandamizwa na Kontena ambalo lilikuwa limebeba Tumbaku katika eneo la Nanenane mkoani humo hii leo.

 

 

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa ajali hiyo imetokea hii leo Agosti 17, 2020 majira ya saa 3:00 asubuhi, ambapo gari aina ya Costa ilikuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro na ndipo ilipolivagaa Lori hilo ambalo lilikuwa limepata hitilafu iliyopelekea Tela lake kukatika na hivyo kuziba njia yote.

 

"Tela hilo lilikatika hivyo kusababisha Tela lililokuwa limebeba tumbaku kukata barabara yote na ndipo gari aina ya Costa iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam iliweza kuingia ubavuni kabisa mwa hilo Tela, tumeokoa jumla ya watu 6 wamepelekwa Hospitali na hali zao ni nzuri, lakini pia tumetoa watu 4 ambao walikuwa mbele kabisa na walikuwa wamekandamizwa na hali zao ni mbaya" amesema Kamanda Mutafungwa.

 

 

Aidha Kamanda Mutafungwa amesema kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.

Maalim Seif Arejesha Fomu za Urais ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)

WhatsApp_Image_2020-09-09_at_8.33.47_PM.jpeg

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amefika katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kurejesha fomu yake leo ambapo ni mwisho wa zoezi hilo na wagombea walitakiwa kuzirudisha kabla ya saa 10 jioni.

TANZIA:RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMINI J. MKAPA AMEFARIKI DUNIA

w1280 p1x1 former tanzania president benjamin mkapa

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa ambae amefariki wakati akiwa anapatiwa matibabu Hospitali Jijini Dar es salaam.
#RIPMzeeMkapa🙏🏼

Viwango vya kubadilishia pesa nchini , Dola, Euro, Kwacha, Ksh, Pound

 
Good morning, karibu ufahamu viwango vya kubadilishia fedha nchini kutoka Benki Kuu ya Tanzania leo September 1, 2020, shuka chini kutazama wamekuwekea viwango vya fedha kwa mataifa 46 kote Duniani
 
 
 
 
 

Page 10 of 184