Local News

Rc Arusha: awataka wanawake kushiriki siasaMkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Kimanta amewataka wanawake kushiriki katika masuala ya siasa na uongozi ili kuweza kuibadilisha jamii kwa kuwa wanawake wana uwezo mkubwa katika masuala ya uongozi kuanzia ngazi ya familia na nguzo ya mabadiliko.

Rc Kimanta ameyazungumza hayo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa mradi wa wanawake katika uongozi na ushiriki katika siasa ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania(TAMWA) na Kuwakutanisha Waandishi wa Habari 50 kutoka Mikoa 17 nchini.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwasihi Waandishi wa Habari kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya dunia katika Tasnia ya Uandishi wa Habari.

WATUMIAJI WA SMARTPHONE HATARINI KUPATA KANSA

bigstock-Mobile-Apps-111905597-660x400.jpg

Watumiaji wa simu janja nchini (smartphone) wanatajwa kuwa hatarini zaidi na kuathirika na mionzi iwapo watatumia simu zao kuzungumza zaidi ya dakika tano bila kupumzisha huku wakiwa na uwezekano wa kupata maradhi ya saratani mbalimbali na matatizo mengine ya kiafya ikiwemo upofu.
Akizungumza na Safari Media Mtafiti wa Afya ya Mionzi kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Kanda ya Kusini Machibya Matulanya amesema kuwa watumiaji hao wa smartphone wako hatarini zaidi kuliko wanaotumia simu za vitochi kwa kuwa smartphone zinamionzi mara 1000 kuliko vitochi.
Machibya anashauri kuwa watu wanaongea na simu kwa muda mrefu kutumia spika ya nje au spika za maskio ili kuepuka madhara na kutoweka simu kichwani wakati wa kulala.
Aidha anawataka kuchua tahadhari kubwa pindi wanapotumia simu zao hasa zinapokuwa na kiwango cha chini ya asilimia kumi cha chaji kwani kitendo hicho kinaweza kuwasababishia matatizo makubwa ya kupata saratani.

WIZARA YA KILIMO YAHIMIZA UADILIFU KAZINI

WhatsApp Image 2020 09 29 at 15.28.04 2

Watumishi wa Wizara ya Kilimo wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa wito huo leo mjini Morogoro wakati alipofungua mafunzo ya siku nne kwa wakuu wa taasisi, bodi na wakala chini ya wizara kuhusu kamati za kudhibiti uadilifu.

Kusaya amewataka watumishi wote kuwa waadilifu ndani ya mioyo yao ili watende kazi walizokabidhiwa kama dhamana ya kuhudumia umma bila upendeleo na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Waziri Mkuu awataka kumuenzi Mark Bomani

WhatsApp Image 2020 09 14 at 19.44.29

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza mazishi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hayati Mark Bomani kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na amewataka Watanzania wamuenzi kwa kuuishi utumishi wake uliotukuka wakati wa kupindi chote cha uhai wake.

Ameyasema hayo leo wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Hayati Bomani kwenye viwanja vya Karimjee na baadaye katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Serikali imepokea msiba huu kwa huzuni na mshtuko mkubwa.

Waziri Mkuu amesemma kati ya mwaka 1965 hadi 1976 aliteuliwa kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo nafasi ambayo aliitumikia kwa uaminifu, uadilifu na umahiri mkubwa na alifanikiwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha sekta ya sharia inaimarika

Kamusi ya kwanza ya Lugha ya alama ya Kidijitali yazinduliwa hapa nchini

IMG-20200927-WA0001.jpg

 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua Kamusi ya kwanza ya lugha ya alama ya kidijitali yenye lengo la kupunguza changamoto ya mawasiliano katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi viziwi. 

Akizindua kamusi hiyo Mkoani Tabora, katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi yenye kauli mbiu “Kuhakikisha upatikanaji wa haki za binadamu kwa Viziwi”, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ave Maria Semakafu amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa makundi yote yenye ulemavu kupata elimu na huduma nyingine za kijamii. 

 

Dkt Semakafu amesema pamoja na maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu, kundi la viziwi lilikuwa limeachwa nyuma huku changamoto kubwa ikiwa ni mawasiliano na kutokuwepo kwa walimu wa kutosha hasa katika ngazi ya sekondari ndio maana imeandaa kamusi hiyo kuwe na lugha moja ya alama na kutoa mafunzo kwa walimu wanaofundisha katika shule zinazopokea watoto viziwi. 

Malipo ya Korosho yafanyike ndani ya siku 30

_109477537_1c271490-d55d-4992-9849-4e732a5a963f.jpg

Serikali imetoa siku 30 kwa uongozi wa mkoa wa Mtwara kuhakikisha inafuatilia wakulima na wadau wengine wanaodai fedha za malipo ya korosho kwa msimu wa mwaka 2018-2019 wanalipwa madai yao kwa madai kuwa serikali imetoa Bilion 401 kwa ajili ya malipo ya korosho mkoani mtwara.

 

Agizo hilo limetolewa na Makamu wa rais na mgombea mwenza wa chama cha mapinduzi CCM Samia Suluu Hassan akiwa katika mikutano ya kampeni jimbo la ndanda, wilayani masasi katika baada ya kukutana na bango yaliyobebwa na wananchi yanayoelezea malamiko hayo na viongozi wa chama kuthibitisha kilio hicho.

Awali akitolea ufafanuzi wa malalamiko kwa wakulima hao mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mtwara Yusuph Nannila amesema serikali imetoa fedha hizo kwa awamu mbili ya kwanza ikiwa shilingi Bilion 389.7 na ya pili shilingi Bilion 20 kumalizia malipo yote lakini anashangazwa kutowafikia wahusika.

 

Mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan leo hii anafanya mikutano mitatu ya kampeni katika jimbo la ndanda,lulindi na masasi akinadi ilani ya chama cha ccm pamoja na utekelezaji wa mipango ya serikali ana kutolea majibu ya baadhi ya changamoto.

MINADA YA KOROSHO KUANZA OKTOBA 2 MTWARA

hqdefault.jpg


Minada ya korosho inatarajia kuanza Oktoba 2, mwaka huu Mkoani Mtwara kwa vyama vikuu vya TANECU na MAMCU na kuendelea katika vyama vikuu vingine kwa mujibu wa ratiba.
Akiongea na wanahabari Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho nchini (CBT) Juma Yusuph ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa walizopokea kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, ghala kuu za minada zitaanza kufunguliwa tarehe 21 Septemba,2020 kwa ajili ya kupokea koroshi kutoka AMCOS.
Katika hatua nyingine amesema kuwa maandalizi ya msimu mpya wa mauzo ya korosho mwaka 2020/2021 yamekamilika kwa asilimia 95 huku ikitoa muongozo na utaratibu wa uuzaaji korosho kwa msimu huo ambao njia mbili zitatumika ikiwa ni uuzaji kwa njia ya mtandao (TMX) na sambamba na mfumo wa stakabaadhi.

 

MGOMBEA UBUNGE CCM MTWARA MJINI AOMBA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI

_MG_1215.jpg

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Hassan Mtenga amemuomba makamu wa Rais na mgombe mwenza wa urais wa chama hicho kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Amezitaja changamoto zinazowakabili wananchi hao kuwa ni upungufu wa madaktari kunakopelekea hospitali kushindwa kuhudumia ipasavyo.
Changamoto nyingine ni upungufu wa magari ya wagonjwa, ubovu wa miundombinu katika kata zaidi ya tatu ikiwemo kata ya magomeni.

Uwepo wa changamoto katika stendi ya mabasi ya mkanaledi kama gharama kubwa za kuunganishiwa huduma za umeme, kutokuwepo kwa shule ya msingi na sekondari ya mfano pamoja na kuwepo kwa migogoro ya ardhi na kutolea mfano mgogoro uliopo baina ya uwanja wa ndege na wakazi wa mtawanya

Page 9 of 184