Local News

MENEJA kampeni wa mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sengerema, Deogratius Medard (42), mkazi wa Kata ya Ibisabageni ktika Wilaya ya Sengerema,amefariki dunia akidaiwa kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu. Marehemu huyo alikuwa meneja kampeni wa mgom


 MENEJA kampeni wa mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sengerema, Deogratius Medard (42), mkazi wa Kata ya  Ibisabageni ktika Wilaya ya Sengerema,amefariki dunia akidaiwa  kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.Marehemu huyo alikuwa meneja kampeni wa mgombea ubunge wa CCM, Hamis Mwagao Tabasamu,alifariki dunia ghafla kabla ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo cha Medard, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema, tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:35 jioni katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema kuwa mtu mmoja Deograrius Medard alifariki dunia.

Alisema marehemu ambaye ni meneja kampeni wa mgombea wa CCM kwnye Jimbo la Sengerema Hamis Mwagao Tabasamu, kabla ya kufikwa na mauti alilalamika kuumwa tumbo baada ya kula chakula (makandekwa chai) na akalamika kukimbizwa hospitali lakini apoteza maisha kabla ya kupata tiba.

Muliro alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho kama kimesababishwa na sumu na ni sumu aina gani.

Mbali na uchunguzi pia linaendelea na mahoajino na watu kadhaa waliokuwa na marehemu Medard kwenye kampeni kabla ya kifo ili kubaini chanzo halisi cha kilichosababisha meneja kampeni huyo wa mgombea wa CCM.

Aidha jeshi hilo mkoani humu limesema limejipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu na kuwataka wananchi wajitokeze kupiga kura Oktoba 28, bila hofu.

Kamanda huyo wa polisi alisema kampeni zinaendelea vizuri na hkuna matukio makubwa ya kutisha yaliyotokea mkoani Mwanza kwani jeshi hilo limejipanga kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo muda wote ili kuwawezesha wananchi kupiga kura.

Alisema jeshi hilo halitamvumilia mtu au kikundi chochote chenye mipango ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwenye mchakato huo wa uchaguzi mkuu wa 2020 na watakaothubutu watashughuliwa kwa mujibu wa kisheria.

Siku ya uchaguzi hakutakuwa na usafiri wa boti wala meli Zanzibar



Ikufikie hii kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) imetangaza kusitisha safari zote za Boti na Meli za abiria na mizigo Jumatano ijayo, Oktoba 28, 2020 ili kutoa fursa kwa Wananchi kupiga kura.

MAMCU WAUZA ZAIDI KILO MILIONI 5

W
akulima wa zao la Korosho wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi, Mtwara Co-operative Union-MAMCU, wamekubali kuuza Korosho zao kwa bei ya juu ya Shilingi 2,607 na bei ya chini shilingi 2,439 kwa Korosho zilizopo katika Maghala ya Micronix, Ketikamba na Mtandi Masasi.

Kulingana na Meneja wa Mkuu wa MAMCU Ndug. Potency Rwiza amesema kuwa korosho kilo 5,526,113 Milion zimeuzwa kati ya kilo 6,975,897 Milion zilizokusanywa.

Aidha Rwiza amefafanua kuwa zaidi ya kampuni 40 zimeonesha nia ya kununua korosho ingawa ni kampuni 14 tu zilizoweka kinga ya dhamana katika msimu huu.

Akizungumza katika mnada huo Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba amesema kuwa msimu wa mwaka 2020/2021 umeweka historia katika mauzo ya korosho baada ya kutumika kwa mfumo wa aina mbili wa kawaida na wa kidigitali.

Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wakulima wanauza korosho zao zote na kupata bei nzuri sokoni ndio maana serikali ikaja na njia mbili ili nchi ambazo mipaka yake imefungwa ziweze kuagiza korosho hizo kwa njia ya mtandao.