Local News

RC Mtwara “Wadau changieni Ndanda FC”


Wadau wa michezo Mkoani Mtwara wametakiwa kuichangia timu ya Ndanda FC inayoshriki Ligi daraja la kwanza, ili kuinusuru kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili.

Wito huo pia umetolewa na mlezi wa timu ya Ndanda FC ambaye pia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, wakati akizungumz na waandishi wa habari Ofisini kwake December 2, 2020.

Mlezi huyo ameeleza kuwa timuhiyo imekuwa na matokeo yasiyoridhisha uwanja, hali ianayochangiwa na Club kutokuwa na uwezo wa kuwalipa mishahara wachezaji wake.

RC Byakanwa ametoa wito kwa wanachi  pamoja na wadau wengine kutoka maeneo mbalimbali ya  Mkoani Mtwara kujitokeza kuichangia timu ya NDANDA ili waweze kuinusuru na hali mbaya ya kiuchumi iliyoikumba.

Amewataka wale wote wenye nia njema ya kuichangia timu ya NDANDA FC kuwasilisha michango yao kupitia akaunti ya CRDB 0150328948001 NDANADA SPORTS CLUB au kupitia Mpesa no 0757858417.

“Mimi Byakanwa mlezi wa timu ya Ndanda nawatangazia kuwa hali ya Ndanda kifedha ni dhoofu bini hali,mimi Mkuu wa Mkoa nimefanya kila hatua nimejitahidi na kamati yangu niliyounda  Naomba nitoe wito kwa wadau na wananchi wote wa Mtwara tujitokeze kuichangia Ndanda’’RC Byakanwa.

MAJALIWA TENA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua tena Mbunge wa Ruangwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sasa Wabunge wanasubiriwa kuthibitisha uteuzi wa jina hilo la Waziri Mkuu Mteule ambalo Rais ameliwasilisha Bungeni.

Kanuni za kuandaa kitalu cha mbogambogaTengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m (ama urefu unaoona wewe kuwa unakufaaa ila tu upana ubaki kuwa 1mita) . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.

Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.

Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati wa kusia ili miche isisongamane.

Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.

Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota .

Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.

Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani.

Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.

KUMBUKA:siku za ukaaji wa mbegu kitaruni inategemeana na aina ya mbegu ama zao.

JPM amwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, atoa neno kwa Wakuu wa mikoa na wilaya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watendaji ndani ya serikali kuchaopa kazi na kuachana na wasiwasi wa kuhisi atawaondoa.Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 9, 2020. kwenye hotuba yake baada ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi akila kiapo mbele ya Rais Magufuli

"Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, kama nilikuteua uwezo si bado ni ule ule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao'', amesema - Magufuli.
"RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama 'performance' yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba Mh Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa", - ameongeza Rais Magufuli.

Marekani kuanza utoaji wa chanjo ya COVID mwanzoni mwa Desemba
Marekani inataraji kuanza utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa juu wa afya katika serikali ya Marekani. Kuanza kutolewa kwa chanjo kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika mapambano ya virusi hivyo ambavyo vimegharimu maisha ya watu zaidi ya milioni 1.4 duniani kote ikiwemo 255,000 Marekani pekee.

Chanjo mbili zinazoongoza moja kutoka kampuni ya Kimarekani Pfizer na mshirika wake kampuni ya Ujerumani BioNTech na nyingine kutoka kampuni ya Moderna, zimeonyesha ufanisi wa asilimia 95 wakati wa majaribio. Mkuu wa mpango wa chanjo wa Marekani Moncef Slaoui, amesema takribani Wamarekani milioni 20 huenda wakapatiwa chanjo ndani ya mwezi Desemba pekee. Kampuni ya dawa ya Pfizer tayari imeomba kibali cha matumizi ya dharura kutoka mamalaka ya chakula na dawa ya Marekani FDA.