Local News

MV Mwanza kukamilika mwakani


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho   amesema ujenzi wa  Meli ya Mv Mwanza Hapakazi tu ambao hadi sasa umefikia asilimia 74 utakamilika baadaye mwakani.

 
Waziri Chamuriho ameyasema hayo leo jijini Mwanza alipokuwa akikagua ujenzi wa meli hiyo ya kisasa  inayojengwa na Kampuni ya Gas Ente kutoka Korea ya kusini ikishirikiana na Kaang Nam Corperation pamoja na Suma JKT. Aidha Waziri Chamuriho amesema ujenzi wa meli hiyo ni moja  ya miradi mikubwa minne inayotekelezwa na   kampuni ya huduma za Meli  Nchini (MSCL) na kusimamiwa na  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. 

Rais Samia awashukia wabunge kuhusu mijadala isio na tija kwa taifa

Rais wa Tanzania,   Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mijadala inayoendelea bungeni ya kumlinganisha na mtangulizi wake,   hayati John Magufuli.

Rais Dkt. Mwinyi awasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanziba akitokea kisiwani Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongozana na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana  alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar, akitokea Kisiwani Pemba baada ya kumaliza ziara yake ya Siku mbili Pemba.(Picha na Ikulu)
 

DMX KUZIKWA APRIL 25, JIJINI NEWW YORKAliyekuwa Meneja wa marehemu rapa #DMX, Steve Rifkind amethibitisha kuwa zoezi la kuaga mwili wa DMX limepangwa kufanyika katika ukumbi wa Barclays Center mjini Brooklyn New York, April 24 mwaka huu.

Siku itakayofuata (April 25), familia ya #DMX na marafiki zake wa karibu watasheherekea maisha ya rapa huyo kwenye mazishi ya faragha ambayo yatafanyika Kanisani mjini New York.

#DMX alifariki dunia April 9 mwaka huu katika hospitali ya White Plains kufuatia kulazwa kwa takribani wiki moja mara baada ya kupata shambulio la moyo kwa kuzidisha dawa za kulevya akiwa nyumbani kwake.

IGP Sirro azindua kitabu cha muongozo wa kuzuia na kufichua uhalifu


MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na uvunjifu wa amani ikiwa pamoja na kuacha kujiingiza tena kwenye matukio ya uhalifu na badala yake wajikite katika kuleta maendeleo kwenye jamii.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua kitabu cha muongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kitabu ambacho kinalenga kutoa dira hasa katika utekelezaji wa mpango wa Polisi kata kupitia mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii.
 

Sababu ya watendaji kukaa maofisini tu, yatajwaMhadhiri  kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. George Kahangwa  amesema viongozi  wanaohitaji kukumbushwa kuhusu kuwa na mpango kazi wanalikosea taifa.


Akizungumza katika Kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio Dkt.Kahangwa amesema kuwa kutoikujua kuhusiana na mpango kazi ndio chanzo chakuwa na watendaji wasiojua wana wajibu gani wa kutimiza kwa taifa matokeo yake hawana la kufanya zaidi kukaa maofisini.
“Suala la mpango kazi halipaswi kiongozi akumbushe ni utaratibu wa kawaida wa kila ofisi hawa wanaohitahji kukumbushwa kuwa na mpango kazi kwa kweli wanalikosea taifa na ndio maana watu wakati mwingine hawajuui wafanye nini”  amesema Dkt. Kahangwa
“Mpango kazi ni jambo la kusisitiza sana kwani mambo ya mpango kazi yanaaibisha yakiwa yanazungumziwa katika ngazi za juu ilhali kuna viongozi ambao  wapo wanaotakiwa wawakague wenzao wa chini kuhusiana namipango kazi yao” ameongeza Dkt. Kahangwa  
Aidha Dkt.Kahngwa amesifu tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli  kuhusiana na kufundishwa histori ya kwetu ambapo amesema kufanya hivyo kutasaidia kizazi hadi kizazi  kujua tunapotoka  na jambo tunalolifanya leo msingi wake ni upi kuliko kuwafundisha vitu ambavyo haviwakumbushi uzalendo wala  chimbuko lao.

MAMCU YAFANYA MKUTANO WA KUCHAGUA VIONGOZI LEO


WAKULIMA wa Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Masasi-Mtwara( MAMCU) hii leo April 21 – 2021 wanafanya mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wenye lengo la kuchagua viongozi wa bodi wa Chama hicho ikiwemo kusoma mapato na matumizi.  

Mkutano huo unafanyika mkoani Mtwara katika ukumbi wa chuo cha ualimu Mtwara.
  Chama kikuu Cha Mamcu kinaundwa na vyama vya msingi( Amcos) zipatazo 165 kutoka wilaya za Masasi , Mtwara na Nanyumbu.

JAFO AZINDUA SOKO LA KISASA CHUNO,MTWARA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amefungua rasmi soko la kisasa la chuno lilliopo Kata ya Chuno Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara. Soko ambalo ujenzi wake umegharimu pesa za kitanzania zaidi ya bilioni tano.

Page 6 of 184