Local News

Rais Samia akizindua mradi wa maji Misungwi mkoani Mwanza

WhatsApp-Image-2021-06-14-at-2.12.35-AM-1-950x633.jpeg

Rais Samia Suluhu leo ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza ikiwa ni siku ya pili, mapema na muda huu anazindua mradi wa maji Misungwi ambao utahudumia wakazi wa kata ya Misungwi na Igokelo wenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 13.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona (COVID -19) nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud Ikulu Jijini Dar es

Capture

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona (COVID -19) nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2021.

IGP Simon Sirro amvalisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamdun

1

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kulia) akimvalisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamdun kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya Mhe. Rais kumpandisha cheo kuwa kamishna wa Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimkabidhi Kamishna wa Polisi CP Salum Hamdun, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kitabu cha Muongozo kinacholiongoza Jeshi la Polisi baada ya kumvalisha Cheo cha Ukamishna kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya Mhe. Rais kumpandisha Cheo kuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ndogo ya Polisi jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi

 

Waziri Mkuu Majaliwa akabidhi magari ya wagonjwa kwa Wabunge

WhatsApp Image 2021 06 01 at 5.11.25 PM 1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe kwenye hafla ya kukabidhiwa magari ya wagonjwa wabunge, kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Juni 1, 2021.  Kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto,  Dkt. Dorothy Gwajima, wa nne kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, kulia ni Mbunge wa Liwale, Zuberi Mohammed Kuchauka  na wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa Global Fund,  Nelson Msuya. Magari hayo yaliyopatikana kwa ufadhili wa Global Fund yamegharimu sh. 2, 240,000,000/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Sakata la Simba v Yanga, Mashabiki kurudishiwa tiket zao

Bashungwa

Waziri Bashungwa ameagiza kituo cha Kitaifa cha Data kinachosimamia N-card kuwarejeshea tiketi zao kwenye mfumo wa kadi za kuingilia uwanjani Mashabiki wote wa Simba na Yanga 43,947 ili siku ya kurudiwa mechi wakae uwanjani eneo lilelile walilolilipia awali.

TOP STORIESRais Samia amuondoa Kamanda mpya DSM amteua kuwa DCI

WAMBURAAAAAAAA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Camilius Wambura, na kuwa Kamishna wa Polisi (CP) ambapo pia amemteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). 

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kueleza kuwa uteuzi huo umeanza jana Mei 30, 2021.

 

Mei 17, 2021, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha Wambura kutoka kuwa 'Chief of Operations Upel' kuu Dodoma na kumhamishia Dar es Salaam kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum akichukua nafasi ya SACP Lazaro Mambosasa.

 

Mchezo wa Simba v Yanga kurudiwa


Makubaliano yamefikiwa kwenye kikao kilichoongozwa na Waziri Bashungwa kwamba mechi ya Simba na Yanga irudiwe "Wizara inaliacha swala hili katika taratibu za TFF na Bodi ya Ligi ili wakae haraka iwezekanavyo na kutoa tarehe ya kurudiwa kwa mechi hiyo"
 

Page 5 of 184