Local News

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO NEWALA (PROSPERITY AGRO )

WhatsApp_Image_2021-07-25_at_17.53.22.jpeg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizindua kiwanda cha kubangua Korosho cha kampuni ya Prosperity Agro Industries kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara. Julai 25,2021

NEEMA KWA WAKULIMA WA KOROSHO, SULPHUR KUTOLEWA BUREE

HZGXCHZGX.png

Katika siku 100 alizokaa madarakani Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha dhana yake ya kuliinua zao la korosho kwa Mikoa ya kusini Tanzania baada ya kurusu salfa zitolewe bure kwa wakulima.Lengo likiwa ni kuongeza tija kwa kulima katika zao la korosho ili liweze kuinika kichumi.
Akieleza hayo Mkurugenzi wa Mtendaji wa kampuni ya prosperity Agro LTD Haroun Maarifa amesema wanayofuraha kubwa kwa kuleta sarufa kwa wakati na amewaomba wananchi kutumia kwa matumizi sahihi vile vile ameishukuru serikali kwa kuwaona wananchi wa zao la korosho.

 

 

Milioni 100 kujenga nyumba ya waalimu, Ugala Nsimbo

IMG 20210716 WA0003

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu alisema Serikali imejiwekea mkakati katika Sekta ya Elimu kwa kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa waalimu wanaofanyakazi katika maeneo magumu na mbali kufikika Aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara katika shule ya Sekondari ya Ugala River iliyopo katika kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi Waziri Ummy alisema katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia Serikali imejikita katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya waalimu wanaotoka mbali kupata maeneo ya kuishi. “ Wapo waalimu ambao wanatoka mbali mfano mzuri ni hapa shule ya Sekondari Ugala River yupo mwalimu ametokea Kilimanjaro na kaamua kuja kufanyakazi katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, Ni wajibu wa Serikali na wananchi wa maeneo husika kuhakikisha wanaboresha mazingira ili waweze kubaki muda mrefu katika maeneo wanayofanyia kazi.” Alisema Mhe Ummy Alisema Serikali inawatia moyo waalimu wote ambao wanafanyakazi katika maeneo magumu hasa katika kata za mbali na kuahidi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiah Hassan Suluhu itawekeza katika kuboresha mazingira ya watumishi nchini Kuhusu Nyumba za waalimu katika Shule ya Sekondari Ugala RWaziri Ummy alisema katika kuunga mkono juhudi za wananchi Serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi ambayo itachukua familia nne kwa pamoja. Lengo ni kuwatia moyo waalimu wanaofanyakazi katika maeneo ya mbali Kuhusu ajira za waalimu wapya alisema Selikali ilitoa kipaombele kwa Halmashauri zenye maeneo yenye changamoto na maeneo ya mbali kufikika , jambo hili limetekelezwa kwa asilimia 100 ambapo kwa shule ya Sekondari ya Ugala River imepata waalimu wa Sayansi 3. Aidha, amesema Serikali ya awamu ya sita imeamua kujikita katika kuimarisha maeneo magumu kama Halmashauri ya Nsimbo ambapo waalimu wapya wa Sayansi 26 wamepangwa katika Halmashauri hiyo

Basi lagonga nyumba Mwanza

WhatsApp-Image-2021-06-30-at-10.34.10-1024x683.jpeg

Basi kampuni ya Ulamaa T 330 DGB ililokuwa likisafiri kwenda Arusha kutokea Mwanza limepata ajali alfajiri ya leo kwa kuacha njia na kugonga nyumba eneo la Mkolani darajani Mwanza.

Imeelezwa kwamba ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na Watu 6 ambapo hakuna taarifa za kifo bali Majeruhi tu ambao wamepelekwa Hospitali ya Butimba.

Chanzo cha ajali kinaelezwa kuwa ni baada ya Dereva wa Basi kulikwepa gari dogo kulikosababisha gari kuacha njia baada ya kushindwa kulimudu, taarifa zaidi kukujia

Mwenge wa Uhuru wazindua miradi ya maendeleo mitatu ya Bilioni 1.1

4_12.JPG

UMLA ya miradi mitatu ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 Wilayani Sikonge imezinduliwa na Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021.

Miradi hiyo inajumuisha Sekta ya viwanda, elimu na Maji.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge John Palingo alisema hayo jana wakati wa mbio hizo wilayani humo na kusema kati ya fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 37.8 ni mchango wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Shilingi bilioni 1.1 ni mchango wa Serikali Kuu, Wananchi wamechangia Shilingi laki 2.6.

Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo inasema “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji”.

Alisema katika mradi wa kwanza Mwenge wa Uhuru umeka Jiwe la Msingi ujenzi Kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki ambacho hadi kukamilika kitagharimu milioni 757.5.

Pallingo alisema kati ya fedha hizo Serikali kuu imechangia milioni 719 na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imechangia milioni 37.8.

Watu 7 wamepoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa kwenye ajali Morogoro

Capture_1.PNG

Watu 7 wamepoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea eneo la nane nane Morogoro ikihusisha magari matatu, Toyota Coaster lililogongana na Toyota Cresta T563 ASA na baadaye Coaster kugongana uso kwa uso na lori namba T658 DJZ. 

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye alitaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Fortunatus Muslim na askari wengine wakiwa eneo la tukio

''Gari la abiria aina ya Toyota Costa lilitaka kulipita gari dogo aina ya Toyota Cresta  ambapo gari hilo lilipoteza uelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Dangote na kusababisha vifo vya watu watano huku majeruhi wakikimbizwa hospitali kwa matibabu,'' - amesema Kamanda Muslim.

Magari yaliyohusika kwenye ajali

Naye mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando  amezungumzia tukio hilo na kutoa rai kwa madereva kufuata kanuni na sheria za barabarani pia akiwaasa abiria kuchukua tahadhari hasa wanapoona mwenendo wa dereva hauridhishi ili kuepuka ajali kama hizo mbazo zinapotea nguvu kazi ya taifa huku mashuhuda wa tukio hilo wakielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea.

Matokeo ya kidato cha sita na ualimu 2021 haya hapa

matokeoo_1.png

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Sita  mwaka 2021 pamoja na matokeo ya mtihani wa ualimu.

Bofya Hapa chini Kutazama

👉👉MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2021

 

Maafisa Ugani Wote Lazima Wawe Na Mashamba Darasa-Majaliwa

1_1.jpg

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wahakikishe Maafisa Ugani wote nchini wanakuwa na mashamba darasa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakulima katika maeneo yao.

“Maafisa Ugani lazima wawe mashamba kwa ajili ya kufundishia wakulima na Afisa Ugani anayeshindwa kuonesha shamba huyo hafai kuwa Afisa Ugani.”

Ametoa agizo hilo jana (Jumapili, Juni 13, 2021) wakati akizungumza na wadau wa zao la alizeti katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mafunzo ya Kanisa Katoliki, Mkoani Singida.

Waziri Mkuu alisema wananchi waliacha kulima kwa sababu elimu ilikuwa haiwafikii, hivyo amewaagiza Wakuu wa Wilaya katika maeneo yote yanayolima alizeti wasimamie uundwaji wa vikundi vya wakulima wa zao hilo. “Vikundi ndio njia rahisi ya kuwafikia wakulima iwe kwa kuwapa elimu au mikopo.”

“…Hakikisheni mnakuwa na kanzi data za wakulima katika maeneo yenu. Kanzi data hiyo itawawezesha kujua idadi ya wakulima, ukubwa wa mashamba yao pamoja na mahitaji yao. Pia jengeni utaratibu wa kuwatembelea wakulima ili kujua changamoto zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa mikoa yote nchini waandae mpango mkakati wa kuendeleza mazao ya mafuta na kuuwasilisha Wizara ya Kilimo kwa ajili ya uratibu, usimamizi na ufuatiliaji. “Na kila kiongozi anapofanya ziara katika wilaya asomewe taarifa kuhusu hatua waliyofikia.”

“Halmashauri za Wilaya zitenge maeneo ya kuzalisha mbegu bora na kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja (Block farms) ili kuongeza uzalishaji na kurahisisha utoaji wa huduma za ugani, mitaji na upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya mafuta ya kula.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alizielekeza taasisi za utafiti wa masuala ya kilimo ziendelee kufanya tafiti za udongo ili kubaini ni aina gani ya mbegu zinazofaa kupandwa kwenye eneo husika. Amesema tafiti zinawawezesha wakulima kupanda mbegu sahihi katika mashamba yao, hivyo kupata mavuno mengi na bora.

Naye, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema wizara imejipanga katika kuongeza uzalishaji wa mbegu bora kutoka tani 344 za sasa hadi kufikia wastani wa tani 2,000 hadi 2,500 kwa mwaka, hivyo ndani ya miaka mitatu ijayo nchi itakuwa imejitosheleza kwa mahitaji ya mbegu za bora alizeti.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge aliiomba Serikali kuunda bodi itakayosimamia mazao ya mafuta ili kuboresha usimamizi wa mazao hayo.  Pia aliishauri Serikali kupitia taasisi zake kama Jeshi la Magereza zianzishe mashamba ya mbegu za alizeti ili kurahisisha upatikanaji wake.

Page 4 of 184