Local News
Yanga yachezea kichapo siku ya Mwananchi
KIKOSI cha Yanga kimepoteza katika mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia.
Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa.
Alianza Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 lilikuja kusawazishwa kipindi cha pili Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.
Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.
Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.
Mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi na licha ya timu yao kupoteza bado waliwashangilia wachezaji wao.
Waziri wa Madini: Fuatilieni tozo zisizo kwenye utaratibu
Naibu Waziri wa Wizara Madini Profesa Shukran Manya ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa na wilaya za Mtwara kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu tozo ambazo hazipo kiutaratibu kwenye idara zinahusika na madini.
Wito huo ameutoa mapema hii leo wakati akieleza dhamira ya ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara, ambapo amesema kwa mwaka 2019 tozo za chumvi zilikuwa zinafika 19 hivyo Serikali imeamua kuzipunguza mpaka kufikia tozo saba.
Aidha amesema licha ya Serikali kupunguza tozo hizo lakini zipo ambazo zinazaliwa ndani ya halmashauri jambo ambalo sio sawa na linapaswa kukemewa.
Mh Profesa Manya yupo katika ziara ya siku mbili leo Agosti 9na 10 na baada ya hapo atakwenda mkoani Lindi
Safari Radio yapata Tuzo
Safari Radio imeibuka washindi wa kwanza Tanzania kwa upande wa Radio kwa kuhamasisha na Kubainisha taarifa muhimu zinazohusu tasnia ya Korosho kwa msimu wa 2020/2021.
Tuzo hiyo imekabidhiwa leo kwa mkurugenzi wa Radio hiyo bwana Haroun Maarifa na Waziri wa kilimo Profesa Aldof Mkenda katika mkutano mkuu wa wadau wa Korosho Tanzania unafanyika leo katika ukumbi wa benki kuu tawi la Mtwara uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Aidha Safari Radio imeibuka washindi wa kwanza baada ya kuwashinda Mashujaa Fm ya mkoani Lindi na Newala fm ambao waliingia nao katika tatu bora.
MKUU WA MKOA WA MTWARA AONGOZA ZOEZI LA CHANJO
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.Jen.Marco Gaguti amezindua rasmi zoezi la kuchanjwa chanjo ya Uviko-19.
Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho wafanyika Mtwara
Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho Tanzania unafanyika leo katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mtwara uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Katika mkutano huo wa mwaka 2021 mgeni rasmi ni Waziri wa kilimo Profesa Aldof Mkenda Waziri wa kilimo.
Pamoja na mambo mengine yatakayo jadiliwa katika mkutano huo ni taarifa ya Mikoa inayo lima zao hilo Tanzania na uchaguzi wa mwenyekiti wa wadau.
Rais Samia aenda Zambia kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mteule Hakainde Hichilema
Rais Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumanne Agosti 24,2021 alipokuwa akielekea Nchini Zambia kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mteule Hakainde Hichilema.
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO NEWALA (PROSPERITY AGRO )
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizindua kiwanda cha kubangua Korosho cha kampuni ya Prosperity Agro Industries kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara. Julai 25,2021
Page 3 of 184