Local News

UKAWA WATAKA UDA IRUDISHWE KWA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea amesema Halmashauri ya Jijiji la Dar es Salaam itahakikisha umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) unarudishwa kwa umma.

Amesema alichokisema CAG kuhusu UDA kimedhihirisha ambacho wamekuwa wakikisema kwa muda mrefu kuhusu mchakato mzima wa uuzwaji wa UDA kuwa ulikuwa wa rushwa, wizi, udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

“Sisi wabunge wa Dar es Salaam kupitia muungano wetu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tumedhamiria kuirejesha umiliki wa UDA kwa umma kwa asilimia 100,” Aidha wamemuomba Rais, Dkt. John Magufuli awaunge mkono katika hili.

Tayari ripoti iliyotolewa mjini Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Assad imeeleza kuwa hisa za UDA zilithaminishwa kwa bei ya Shilingi 744.79 kwa kila hisa Oktoba, 2009 na Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikiwa Shilingi 656.15.

Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa Februari 11, 2011, mnunuzi (kampuni ya Simon Group Limited) ilitakiwa kulipa Shilingi Bilioni 1.14 kwa bei ya ununuzi wa hisa zote. Hata hivyo, mnunuzi alilipa Shilingi milioni 285 pekee katika akaunti namba OJ1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba alipokea kiasi cha Shilingi milioni 320 kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa mwekezaji ambapo kwa mujibu wa Simba, ni ada ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji jambo ambalo linaonesha kuwepo kwa mgongano wa masilahi.

VIONGOZI WA SIASA WATAKIWA KUZINGATIA DEMOKRASIA

VIONGOZI kutoka katika Vyama mbalimbali vya Kisiasa Mkoani Mtwara wamehamasishwa kutumia Elimu ya Demokrasia katika Uongozi ili kutambua Majukumu yao, kuepusha Migogoro na kuleta Maendeleo ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi.FATMA ALLY, katika Ukumbia wa Camp Site Mjini hapa wakati akizungumza katika ghafla ya Wahitimu wa Mafunzo ya Elimu na Demokrasia iliyoandaliwa na Mradi wa SENTER PART unaofadhiliwa na Serikali ya NORWAY unaojihusisha na kutoa elimu kwa makundi mbali mbali ya Viongozi wa kisiasa hapa Nchini.

Amesema mara nyingi kumekuwa kukitokea hali ya muingiliano wa majukumu kwa viongozi wa siasa hususani walio katika ngazi ya chini kama wenyeviti na madiwani kutokana na baadhi yao kutofahamu ukomo wa majukumu, lakini kutokana na mafunzo hayo anaamini yatawasadia katika mambo mengi.

Aidha kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo Bi LUCY AGUSTINO, amesema mradi huo ulianza Mwaka 2011, na Kila mwaka walikuwa wanateuwa wawezeshaji wanane wanane kutoka katika kila chama na kuwapatia Mafunzo mbalimbali ikiwemo ya dhana za Demokrasia na Utawala Bora.

Nao wahitimu wa Mafunzo wameeleza kufurahishwa na kudai kunufahika kutokana Mradi huo ikiwa ni pamoja na kuelewa dhana ya Uongozi bora katika Jamii inayowazunguka.

Rais Magufuli Awaapisha Makatibu Tawala Wapya Wa Mikoa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.

Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Makatibu Tawala walioapishwa ni;

1. Arusha - Richard Kwitega

2. Geita - Selestine Muhochi Gesimba

3. Kagera - Armatus C. Msole

4. Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour

5. Pwani - Zuberi Mhina Samataba

6. Shinyanga - Albert Gabriel Msovela

7. Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi

8. Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini

9. Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara

10. Tanga - Eng. Zena Said

Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.

MKUU WA MKOA WA LINDI HAJARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA TANESCO

Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Lindi limetakiwa kuboresha utendaji kazi wake ili kuondoa hadha na hasara kwa wananchi kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara. Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa Lindi Godfrey Zambi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa fisi-Mkoani hapo. Zambi amesema kitendo cha kukatika umeme mara kwa mara bila taarifa kunachangia uharibifu na kuungua kwa vifaa vya wananchi.

Amesema kwa kipindi chote alichopo mkoani Lindi hajawahi kufaidi na kuona umeme umetulia bila itilafu na kusikitishwa na tukio la siku moja alipoona umeme umekatika zaidi ya mara 12 Zambi amelitoa agizo hilo baada ya wananchi wa Manispaa ya Lindi kulalamikia tanesco kukatika kwa umeme mara kwa mara na kutotoa taarifa ya tatizo hilo kwa wananchi linapotokea. Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Lindi Naomi Mwaipula amesema kukatika kwa umeme kunatokana na kuwepo kwa miundo mbinu chakafu hivyo shirika lianza kufanya marekebisho ya kuondoa miundombinu chakavu na kuweka mipya na zoezi litakamilika mapema ya desemba 2016.

Page 184 of 184