Local News

Marekani kuanza utoaji wa chanjo ya COVID mwanzoni mwa Desemba
Marekani inataraji kuanza utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa juu wa afya katika serikali ya Marekani. Kuanza kutolewa kwa chanjo kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika mapambano ya virusi hivyo ambavyo vimegharimu maisha ya watu zaidi ya milioni 1.4 duniani kote ikiwemo 255,000 Marekani pekee.

Chanjo mbili zinazoongoza moja kutoka kampuni ya Kimarekani Pfizer na mshirika wake kampuni ya Ujerumani BioNTech na nyingine kutoka kampuni ya Moderna, zimeonyesha ufanisi wa asilimia 95 wakati wa majaribio. Mkuu wa mpango wa chanjo wa Marekani Moncef Slaoui, amesema takribani Wamarekani milioni 20 huenda wakapatiwa chanjo ndani ya mwezi Desemba pekee. Kampuni ya dawa ya Pfizer tayari imeomba kibali cha matumizi ya dharura kutoka mamalaka ya chakula na dawa ya Marekani FDA.
 
 

Wachimbaji wadogo 8 wajeruhiwa, Buhemba Mara


Wachimbaji wadogo nane wajeruhiwa kwa silaha za jadi ikiwamo mapanga, visu pamoja na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao katika machimbo ya dhabu ya Irasanilo, Buhemba yaliyopo wilayani Butiama mkoani Mara chanzo kikiwa ni kugombania maduara ya uchimbaji.Wakizungumza baadhi ya majeruhi hao wamesema wakiwa wanaendelea na uchimbaji ndani ya shimo, walivamiwa na kundi la watu ambao walianza kuwashambulia na nondo mawe pamoja na kuwachoma na visu sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumzia tukio hilo mmiliki na katubu wa duara hilo namba tisa A, ambalo limevamiwa, Mwajuma Seif amesema kabla ya tukio hilo duara hilo lilikuwa na mgogoro huku uongozi wa wachimbaji hao wadogo mkoani Mara, wakatoa tamko la kulaani tukio hilo la kikatili kwa wenzao.

 Kamanda wa Jeshi la Polisi na alizungumza kwa njia ya simu na kukiri kuwepo kwa tukio hilo na hapa anaeleza zaidi.

TANZANIA NA MSUMBIJI ZAJADILI HALI YA USALAMAMkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Simon Sirro na Kamanda mkuu wa Polisi wa Jamhuri ya Msumbiji Bernardino Rafael wamekutana leo Mkoani Mtwara na kuzungumzia hali ya usalama katika eneo la mpaka baina ya nchi hizo mbili ambako kumekuwa kukitokea matukio ya uhalifu na machafuko mara kwa mara yanayodaiwa kufanywa na makundi ya kigaidi yenye itikadi za kidini.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha ndani kilichodumu kwa muda wa masaa matatu viongozi hao wamesema kuwa wamekubaliana mambo mengi ikiwa pamoja na kuendesha oparesheni za kijeshi na kubadilishana taarifa ili kuhakikisha wanawanasa wahaalifu hao.

Akianza kuongea juu ya kile walichokubaliana IGP mwenyeji Simon Sirro amesema kuwa wamejipanga vizuri na kujihimarisha ipasavyo na kuahidi kuwa haitachukuwa muda mrefu watawashughulikia, huku akiwataka wananchi waliokimbia maeneo yao katika vijijini vya mpakani kurudi na kuendelea na shughuli zao.

Kutokana na kundi kubwa la vijana wa Tanzania kudaiwa kujiunga na makundi hayo ya kigaidi yenye itikadi za kidini, Sirro amewataka wazazi kujitahidi kuwaonya watoto wao kwa kuwa hawatawaacha salama na kula nao sahani moja.

MAJALIWA TENA