Meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa Arsenal Arsene Wenger mwisho wa msimu. (Kicker - kwa Kijerumani)

Hilo lisipofanyika, Tuchel basi badala ya kwenda Arsenal atajiunga na Paris St-Germain ya Ufaransa, ingawa Chelsea bado wanazisaka huduma zake. (Sportbuzzer - kwa Kijerumani)

Wawakilishi wa Barcelona watakutana na wenzao wa Atletico Madrid siku chache zijazo kwa lengo la kukamilisha makubaliano kuhusu uhamisho wa nyota Mfaransa Antoine Griezmann, 27. (Sport - kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ataihama klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote mwisho wa msimu huku Manchester City na Juventus wakidaiwa kumtaka iwapo klabu yake haitaongeza mshahara wake ambao kwa sasa ni £200,000 kila wiki. (Sun)

Manchester United wanamtaka beki wa Scotland wa miaka 20 anayechezea klabu ya Celtic Kieran Tierney. (Daily Record)

Inter Milan nao wamewapiku Manchester City na Barcelona na kupata saini ya beki Mholanzi Stefan de Vrij, 26, ambaye atajiunga nao kutoka Lazio bila ada yoyote mwisho wa msimu. (Gazzetta dello Sport - Kwa Kitaliano)

Kiungo wa kati kinda wa Manchester City Phil Foden, 17, na kinda anayechezea Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18, waliondolewa kwenye kikosi cha England cha wachezaji wa chini ya miaka 19 wanaocheza michuano ya ubingwa Ulaya baada yao kufika kwa mazoezi wakiwa wamechelewa. (Telegraph)

0768671579

Add comment


Security code
Refresh